FILAMU YA ”THE INTERVIEW” YAVUNJA REKODI YA MAUZO
Kampuni ya Sony imesema kuwa filamu ya ”The Interview” imenunuliwa mtandaoni zaidi ya mara milioni 2 na kuzalisha zaidi ya dola milioni 15 katika siku nne za kwanza.
Aidha kampuni iyo imesema kuwa filamu iyo inayopatika katika
mitandao ya Google, Youtube, Microsoft Xbox Video na katika tovuti yenye
muonekano wa HD hukodishwa kwa muda wa saa 48 kwa dola 5.99 na kuuzwa
kwa dola 14.99.
Takwimu hizi zinaifanya filamu hii iliyochezwa na Seth Rogen
pamoja na James Franco kuvunja rekodi katika kampuni ya Sony kwa mauzo
na kuangaliwa zaidi kupitia mitandao kwa muda wa siku chache zaidi tangu
kutolewa rasmi.
Mapema kampuni ya Sony Pictures ilihairisha mpango wake wa
kuiachia filamu iyo katika siku ya Christmas baada ya kompyuta za
kampuni iyo kudaiwa kuingiliwa na wadukuzi huku Korea ya kaskazini
ikihusishwa katika udukuzi huo. Itazame Trailer yake hapo chini
FILAMU YA ”THE INTERVIEW” YAVUNJA REKODI YA MAUZO
Reviewed by crispaseve
on
18:52
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
18:52
Rating:

Post a Comment