Header AD

PATCHO MWAMBA : SIJAFUMANIWA NA MKE WA MTU NI ALEJI YA MACHO TU!

Pichani Patcho mwamba Kabla na baada ya kupata Aleji
Pichani ni Patcho mwamba Kabla na baada ya kupata kasumba hiyo
Mwanamuziki wa Bendi ya wazee wa Ngwasuma Fm Academia na mwigizaji wa Bongo Movie, Patcho Mwamba amekanusha vikali habari zilizozagaa kwenye mitandao na media mbalimbali akidaiwa kuchezea kichapo baada ya kufumaniwa na mke wa mtu eneo la Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa tovuti ya Global Publishers ilimnukuu Patcho akisema picha iliyozagaa mitandaoni ikimuonyesha ameumuka usoni ni yeye mwenyewe aliamua kuisambaza baada ya kupata aleji ya macho kutokana na kunywa pombe.
Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe” alisema Patcho na kuongeza, ”juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka”.
PATCHO MWAMBA : SIJAFUMANIWA NA MKE WA MTU NI ALEJI YA MACHO TU! PATCHO MWAMBA : SIJAFUMANIWA NA MKE WA MTU NI ALEJI YA MACHO TU! Reviewed by crispaseve on 10:26 Rating: 5

No comments

Post AD