EXCLUSIVE : RAPA EMINEM AKIRI KUJIHUSISHA NA USHOGA
Rapa
Eminem ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kukiri kujihusisha na
mahusiano ya jinsia moja yaani Ushoga wakati alipokuwa akihojiwa kwenye
kipande kifupi cha filamu ya komedi ”The Interview” iliyochezwa na James Franco pamoja Seth Rogen ambayo imetengenezwa na kampuni ya Sony Pictures.
Katika mahojiano hayo, Eminem alipigwa swali kuhusiana na mashairi ya nyimbo zake nyingi kutokea kuwakera watu wazima.
”Sio lazima niimbe vitu ninavyovichukia, zaidi ni kuhusiana na vitu ninavyovihofia”, alisema hitmker uyo wa Monster na kuongeza, ”Pindi naposema vitu kuhisiana na mashoga, au watu wanapodhani mashairi yangu yanawabagua, – ni kwasababu mimi ni shoga”.
”Nawapenda wanaume. Nashangazwa
zaidi pale watu wanaposhindwa kuelewa bado. Namaanisha, ni kama vile
nimekuwa nikicheza aina flani ya mchezo wa mashoga kuchagua wenzi wao”, alisema Eminem kwa utani.
Kwa sasa Filamu ya ”The Interview” inapatikani kwenye
Application ya Google Store na Youtube ambayo kimsingi inaelezea
jitihada za kumuua kiongozi wa Korea kaskazini ‘Kim Jong-Un’ kufuatia
tuhuma zinazoikabili nchini yake ukiwemo wizi wa mtandao katika kampuni
ya Sony Pictures, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na ugaidi.
Itazame Interview iyo hapo chini
EXCLUSIVE : RAPA EMINEM AKIRI KUJIHUSISHA NA USHOGA
Reviewed by crispaseve
on
10:24
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
10:24
Rating:

Post a Comment