Header AD

WAKENYA WAWAFUNIKA WATANZANIA MICHUANO YA TENISI DAR OPEN

DSC_0453
Mmoja wa wadhamini kutoka kampuni ya mawikili ya IMMA ya Dar es Salaam, Alexander Sarac, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania kwa udhamini mkuu wa kampuni ya magari ya CFAO Motors kupitia brandi ya magari ya Mercedes Benz. (Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu

WACHEZA tenisi kutoka nchini Kenya wamewafunika watanzania katika michuano ya kimataifa ya kwanza ya tenisi kwa walemavu (Dar Open ). Michuano hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kesho katika viwanja vya Gymkhana, majira ya saa 10 ambapo washindi watapewa tuzo zao.

Kwa mujibu wa matokeo ya hadi mchana wakati mwandishi wa habari hizi anaondoka viwanjani hapo, mechi saba zilienda kwa wakenya kwa nafasi ya wanaume na wanawake na mbili ndio walishinda Watanzania.

Michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO, Mercedes-Benz na kampuni ya mawakili ya Dar es salaam ya IMMMA imelenga pia kuandaa wachezaji kwa ajili ya mechi za kufuzu michezo ya dunia zinazotarajiwa kupigwa nchini Kenya Februari mwakani.
DSC_0413
Mshiriki wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania, Rehema Selemani akirusha mpira wakati akichuana na mshiriki kutoka Mombasa, Phoebe Masika (hayupo pichani).

Kwa mujibu wa msemaji wa wadhamini wa michuano hiyo Alexander Sarac, michuano hiyo yenye washiriki wanaume 17 na wanawake watano walioitwa kutoka Tanzania na Kenya, imelenga kuwezesha walemavu kuendeleza vipaji vyao vya kucheza tenisi.

Pamoja na kuwa na ushindi dhaifu wa watanzania kocha wa timu ya Tanzania amesema bado ana bunduki zake mbili na ana hakika kesho vikombe vitabaki Tanzania. Fungua dimba ya michuano hiyo ilianzishwa na watanzania Novatus Temba na Moses Sebastian ambapo Temba alimchapa Sebastian kwa seti 2-0; mkenya Itaken Timoi alimvuruga Bernad Antony kwa seti 2-0 huku Mkenya mwingine Peter Mnuve akimtoa Mtanzania Albert John kwa seti 2-0.
DSC_0376
Katika michezo mingine Rajab Abdallah kutoka Kenya alimtoa Adil Hashim kwa seti 2-0 huku Yohana mwila wa Tanzania akimpa taabu Kenya ambaye alimuondoa kwa seti 2-1. Muingereza anayeishi nchini Ian Artetiel alimtoa Mtanzania Voster Peter kwa seti 2-1.
WAKENYA WAWAFUNIKA WATANZANIA MICHUANO YA TENISI DAR OPEN WAKENYA WAWAFUNIKA WATANZANIA MICHUANO YA TENISI DAR OPEN Reviewed by crispaseve on 07:55 Rating: 5

No comments

Post AD