DR.DRE AUPIGA BEI MJENGO WAKE WA KIFAHARI
Pindi
unapokuwa miongoni mwa marapa mabilionea Duniani, huna budi kubadilisha
mazingira kulingana na hadhi yako ilivyo. Mtayarishaji mkongwe wa
muziki kutoka Marekani, Andre Romelle Young ‘Dr.Dre’ ameamua kuupiga bei mjengo wake wa kifahahri uliopo eneo la Hollywood Hills, California.
Dre mwenye umri wa miaka 49, ameuuza mjengo wake huo kwa dola
za kimarekani milioni 32.5 ikiwa ni mara mbili ya bei aliyonunulia,
ambao upo mtaa mmoja na mijengo ya mastaa wenzake kama vile Leonardo
DiCaprio, Keanu Reaves na wengine kibao.
Inasemekana Dre ameamua kuusukuma mjengo huo wenye vyumba 6
vya kulalia, mabafu 8 na vikolombwezo vingine baada ya kufanya ununuzi
wa mjengo mwingine katika kipindi cha kipupwe mwaka jana ambao
ulimgharimu dola milioni 40 na ushee uliokuwa ukimilikiwa na Tom Brady
na mkewe mwanamitindo. Utazame mjengo wake alioupiga bei hapo down
DR.DRE AUPIGA BEI MJENGO WAKE WA KIFAHARI
Reviewed by crispaseve
on
02:29
Rating:
Post a Comment