50 Cent na Tatted Up Holy wakiwa katika interview enzi za mahaba niue
Siku zote mapenzi yanapoanza huwa ni matamu kama asali, ila
mambo hugeuka pale wapendanao wanapoachana kwa shari. Rapa 50 cent
ameamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi baada ya kuanika siri za ndani
za aliyekuwa mpenzi wake. Ishu hiyo inatajwa kusababishwa na tovuti ya Media Take Out
ambayo iliandika habari kuhusiana na mwanamke huyo anayefahamika kwa
jina la Tatted Up Holy na kumtaja kama mchumba wake, kitendo
kilichopelekea kuamsha hasira za rapa huyo na kuanza kuanika maovu yake.
”Mwanamke huyu ni jamvi la wageni”, alisema 50 na kudai
kwamba amewahi kuvunja amri ya sita na mastaa wenzake kibao akiwemo Trey
Songz, Jr Smith na wengineo Baada ya kuona akishambuliwa, Tatted Up Holy aliamua kujibu
mapigo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kudai kuwa enzi za mapenzi
yao alikuwa muaminifu kwa rapa huyo licha ya vipigo vya mara kwa mara
alivyokuwa akiambulia. Unaweza ukamtazama kwa uzuri Ex wa 50 hapo chini
50 CENT AMUITA EX WAKE JAMVI LA WAGENI
Reviewed by crispaseve
on
02:26
Rating: 5
Post a Comment