KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUIKEMEA CUF KUWAITA MAKAFIRI WANAOHAMIA CCM
Katika mkutano huo, Kinana alitumia staili yake ya kuwakataza wananchi kumshangilia akiwataka wamsikilize vizuri maneno aliyokuwa akizungumza kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ambapo alimsifia Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kwa uchapakazi wake kwa kuwaletea maendeleo wananchi katika visiwa vya Pemba na Unguja.
Alisema wakati wa uongozi wake amejenga barabara nyingi za lami, miradi ya maji, Afya na elimu karibu kila kona ya visiwa vya Pemba na Unguja, lakini wakati anafanya mambo yote hayo wapinzani wakiwemo viongozi wa CUF na wafuasi wao wanajifanya hawayaoni maendeleo hayo.
Alisema Serikali YA ccm iliyo chini ya Rais Dk. Shein imepeleka umeme, miradi ya maji na barabara za lami hata katika Jimbo la Mtambwe alikozaliwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.
Kinana amelaani kitendo cha CUF kuwaita makafiri watu wotinginee wanaokihama hicho kwenda CCM na vyama vingine, ambapo ameomba viongozi wa dini kulikemea jambo hilo, akidai hakuna binadamu mwenye haki ya kumwita mwenzie kafiri isipokuwa Mungu.
Pia alikemea vikali tabia isiyo sahihi iliyozuka ya kuwatenga waliokuwa wana CUF na kuamua kujiunga na CCM na vyama vingine, akidai kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote akipendacho.
KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUIKEMEA CUF KUWAITA MAKAFIRI WANAOHAMIA CCM
Reviewed by crispaseve
on
01:18
Rating:
Post a Comment