Header AD

PICHA:MGOMO WA WAFANYABIASHARA IRINGA

Askari  wa FFU  wakizunguka mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa jana kama  njia ya  kulinda amani kwa  wafanyabiashara  ambao  waliendelea  kutoa huduma  baada ya wenzao  kuwa katika mgomo
MOja  kati  ya  maduka  mjini Iringa yakiendelea  kutoa  huduma  mbali ya  wafanyabiashara  wengine  kuwepo katika mgomo  kushinikiza  kuachiwa  huru kwa mwenyekiti wa  wafanyabiashara  Taifa  Bw  Johnson Minja
Maduka  mtaa wa  uhindini mjini  Iringa  yakiwa  yamefungwa jana  kuunga mkono mgomo  wa wafanyabiashara  nchini
Mmoja kati ya  wafanyabiashara  wadogo (machinga) mjini Iringa akiwa amepanga  bidhaa zake  nje ya  duka moja wao  eneo la Miyomboni kufuatilia wafanyabiashara  wenye maduka  kufunga maduka yao kushinikiza  jeshi la  polisi  kumwachia mwenyekiti  wao Taifa ,hapa  ni  kufa kufaana
Wananchi mbalimbali  wa mji  wa Iringa  wakiwa katika  soko  kuu la mjini Iringa  kupata  huduma  zao wakati sehemu mbali mbali huduma  zikiwa  zimesitishwa  kufuatia mgomo  wa wafanyabiashara  nchini
Na matukiodaimaBlog
BAADHI ya  wafanyabiashara   mkoani  Iringa  jana   wamegoma  kuungana na  wafanyabiashara    wenzao nchini  kushiriki mgomo  wa  kushinikiza  jeshi la  polisi  kumwachia  huru mwenyekiti  wao  wa chama  cha  wafanyabiashara  nchini Bw  Johnson  Minja anayedaiwa  kushikiliwa na  jeshi la polisi kwa mahojiano.
PICHA:MGOMO WA WAFANYABIASHARA IRINGA PICHA:MGOMO WA WAFANYABIASHARA IRINGA Reviewed by crispaseve on 01:14 Rating: 5

No comments

Post AD