MKOA WA MBEYA WAIOMBA IDARA YA MAMBO YA KALE KUWAKABIDHI MAKUMBUSHO YA MAMBO YA KALE YA KIMONDO
MKOA wa mbeya umepania kuboresha miundo ya kituo cha mambo ya kale cha Kimondo wilayani Mbozi mkoani hapa iwapo Idara ya Mambo ya kale iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii itakubali ombi la mkoa huo kukabidhi kivutio Halmashauri ya Mbozi.
Hatua
hiyo imekuja kufuatilia ziara ya wanahabari mkoani Iringa
wanaotembelea vivutio vya utalii mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa
kama njia ya kuhamasisha utalii mkoa ya nyanda za juu kusini na
pia kubaini sababu za utalii kutokua kwa kasi katika mikoa hiyo .
Mhifadhi
msaidizi wa kituo cha makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo
wilayani Mbozi Bw Mussa Nsojo alisema kuwa mbali ya watalii wengi
kupenda kutembelea eneo hilo la Kimondo ila miundo mbinu ya eneo
hilo si rafiki kwa watalii kuendelea kutembelea kutokana na
serikali kushindwa kuboresha majengo na eneo hilo kwa ujumla.
Alisema
kuwa kimondo hicho ambacho mwaka kilipoanguka eneo hilo
haufahamiki ila utafiti wake ulianza kati ya mwaka 1930 -1931 na
kubainika kuwa si jiwe la kawaida bali ni sayari iliyoanguka kutoka
angani toka wakati huo kimendelea kupata umaarufu wa watalii
kufika kutembelea eneo hilo japo katika eneo hilo mazingira yake ni
mabovu zaidi.
Mhifadhi
huyo akielezea historia ya kimondo hicho alisema kabla ya
watafiti kubaini kuwa ni kimondo miaka ya nyuma kulikuwa na
wenyeji ambao walikuwa wakiishi eneo hilo na mkazi mmoja
aliyefahamika kwa jina la Harele ambae alikuwa akifanya kazi ya
uhunzi kuweza kubaini jiwe hilo la ajabu wakati akitafuta udongo chuma
kabla ya kumega kipande kidogo na kutengenezea shoka .
Alisema
kutokana na wakati huo chuma kuwa na dhamani kubwa alipeleka
taarifa kwa chifu wa eneo hilo na kulifanya eneo hilo kuwa la
tambiko kabla utawala wa Waingereza kuchukua eneo hilo na
kulihifadhi kabla ya serikali ya Tanzania kupitia idara ya mambo ya
kale kuhifadhi eneo hilo.
MKOA WA MBEYA WAIOMBA IDARA YA MAMBO YA KALE KUWAKABIDHI MAKUMBUSHO YA MAMBO YA KALE YA KIMONDO
Reviewed by crispaseve
on
09:29
Rating:
Post a Comment