WAKAZI : HOMA YA DENGUE ILINIFANYA NIITUNGIE WIMBO
Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo mwenye makazi yake Ukonga jijini
Dar es salaam, Webiro Wakazi amesema kipindi anaandika ngoma yake mpya
‘Dengue Fever’ alikuwa akiumwa ugonjwa huo unaosambazwa na mbu aina ya
Aedes Aegypti ambao ulipata kuwa habari ya mjini.
Wakazi amepasua kwamba, kitu kikubwa alichozungumzia ndani ya
wimbo huo ni kuonyesha ni jinsi gani alivyoshindikana na kupitiliza.
Moja ya mistari katika ngoma hiyo unasema, ”Niite mbu wa mchana A.K.A Dengue Fever’‘.
”Niliumwa Dengue Fever, sikujitangaza lakini niliumwa Dengue Fever, wakati naumwa ndio nikawa natunga haya mashairi”, Wakazi alifunguka kwenye kipindi cha X-Ray ya EFM
Pia msanii huyo amezungumzia experience aliyopata wakati
alipopata shavu la kutumbuiza katika shindano la Big Brother Africa The
Chase mwaka juzi.
”Wanasemaga nabii hakubaliki kwao, kwaiyo mimi nilikuwa nafanyia muziki toka niko nje, nazituma nyimbo za mixtape, lakini nikarudi nikatoa audio na video kali lakini nikaona bado upokelewaji wangu upo so so hivi wa uvuguvugu”, alisema Wakazi
”hasa watu wa nje, kwa sababu nilikuwa najinadi
kwenye mitandao ya kijamii,watu wa nje wao kunipa nafasi kubwa kama ile
kwenda Big Brother, ikanionyesha nachokifanya sio kwamba ni kibaya, sema
labda tuu home watu hawajaelewa, lakini si kwamba mimi hapa sieleweki
, kwa sababu wao wameamua kunielewa kwaiyo ilikuwa na nafasi nzuri sana
kwangu”.
WAKAZI : HOMA YA DENGUE ILINIFANYA NIITUNGIE WIMBO
Reviewed by crispaseve
on
01:55
Rating:
Post a Comment