Kluivert, Edgar Davids, Mandieta kucheza Tanzania Machi 28
Mshambuliaji
wa zamani wa FC Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi Patrick Kluivert
alizungumzia ujio wa magwiji FC Barcelona nchini mwezi wa tatu mbele ya
waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Sports Lounge uliopo jijini Dar
Es Salaam ,Pembeni ya Kluivert ni mwenyekiti wa DRFA Ndugu Almas
Kasongo. Magwiji hao wa Barcelona wanataraji kucheza na wachezaji nyota
wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa mnamo mwezi wa machi tarehe 28.
Mwenyekiti
wa chama cha soka mkoa wa Dar Es Salaam,Almasi Kasongo akizungumza
kwenye mkutano huo katikati na mwakilishi wa FC Barcelona pamoja na
Mwakilishi wa kampuni ya Prime Time Promotions Stuart Kambona ambao ni
waratibu wa mchezo huo.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema leo asubuhi
Timu ya
wachezaji nyota wa zamani wa Barcelona FC watacheza na wachezaji wa zamani wa
Tanzania, Tanzania All Stars Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa jijini.Mwakilishi
wa wachezaji wa zamani wa Barcelona, Patrick Kluivert alisema jana kuwa mechi
hiyo itawahusisha wachezaji nyota wa Barcelona wakiwemo, Edgar Davids, Gaiza Mandieta,
Ludovic Giuly, Francesco Coco na wengine wengi waliopitia klabu hiyo kwa miaka
tofauti.Kluivert
alisema kuwa kikosi chao kina wachezaji nyota ambao ni maarufu duniani na
wanaamini mechi itakuwa nzuri na yenye ushindani mkubwa.
Alisema kuwa
yeye ni mwenyeji sana hapa Tanzania kwani huu ni ujio wake wa tatu na anaamini
kuwa jinsi mashabiki wanapenda sana mpira wa miguu, itakuwa fursa kubwa kwao
kuona vipaji vya zamani ambavyo
vimetukuka.“Ninafurahi
kuja nchini Tanzania kwa mara ya tatu, ni faraja kubwa pia kucheza hapa nchini
kwa mara ya kwanza, naomba mashabiki wa soka wajae uwanjani kuona mpira wenye
ushindani,” alisema Kluivert.
Mwakilishi
wa kampuni ya Prime Time Promotion inayoratibu mechi na ziara ya timu hiyo ya
Barcelona, Stuart Kambona alisema kuwa madhumuni ya mchezo huo ni kudumisha
mahusiano ya kibiashara ya mpira wa miguu baina ya Tanzania na Hispania, kutangaza
utalii na kuendeleza mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili.
Kambona
alisema kuwa pamoja na kucheza soka siku hiyo, ujio wao pia utaitangaza nchi
nje ya mipaka yake na kuleta fursa nyingi hapa nchini.“Wachezaji
wa Barcelona wanataingia nchini siku mbili kabla ya mechi na watakuwa zaidi ya
20, majina ya wachezaji wengine yatatangazwa baadaye, ila tunaomba wadhamini
wajitokeze kufanikisha na kufaidika na mechi hiyo,” alisema Kambona.
Mwenyekiti
wa Chama cha soka cha mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Almasi Kasongo aliwaomba mashabiki wa soka kujiandaa
kuangalia mechi hiyo kwa kufika
uwanjani.
Kasongo alisema kuwa DRFA imefarijika sana kwa ziara hiyo na kuiomba Prime Time Promotion kuhakikisha kuwa inapanua wigo kwa kuandaa mechi nyingi ambazo zitakuwa chachu ya maendeleo ya soka nchini
Kluivert, Edgar Davids, Mandieta kucheza Tanzania Machi 28
Reviewed by crispaseve
on
05:39
Rating:
Post a Comment