SKYLIGHT BAND YAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE NDANI YA NYAMA CHOMA FESTIVAL
Kikosi
cha Skylight Band kikiongozwa na mkongwe wa muziki wa Live Band, Joniko
Flower (kushoto) kutoa burudani kwa mashabiki wake ndani ya viwanja vya
Leaders Club kwenye tamasha la Nyama Choma lilifanyika mwishoni mwa
wiki. Kutoka kulia ni Sam Mapenzi, Aneth Kushaba AK47 pamoja na Sony
Masamba.
Swagga za Skylight Band hii inafahamika kama "Mashauzi" mkongwe Joniko Flower akiwasebenesha mashabiki wake ( hawapo pichani).
Asali ya warembo Sam Mapenzi akifanya yake jukwaani kwenye tamasha la Nyama Choma ndani ya viwanja vya Leaders Club.
Watu weweeeeeeee yani ni full mzuka...pole kwa uliyekosa burudani ya aina yake ndani ya Leaders Club.
Vijana wakilisongesha gwaride la sebene ndani ya Nyama Choma Festival.
Majembe
ya Skylight Band yakiongozwa na Sony Masamba (katikati) kutoa burudani
kwenye tamasha la Nyama Choma ndani ya viwanja vya Leaders Club. Kushoto
ni Joniko Flower na kulia ni Sam Mapenzi.
Warembo wakijinafasi ndani ya Leaders Club kwenye tamasha la Nyama Choma huku Skylight Band ikitoa burudani.
SKYLIGHT BAND YAKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE NDANI YA NYAMA CHOMA FESTIVAL
Reviewed by crispaseve
on
01:37
Rating:
Post a Comment