USELA WAMPONZA CHRIS BROWN, AKATALIWA KUINGIA CANADA, ALAZIMIKA KUVUNJA MATAMASHA YAKE
Mwanamuziki
nyota wa Marekani, Chris Brown ameendelewa kuandamwa na gundu baada ya
kukataliwa kuingia nchini Canada na kulazimika kukatisha matamasha yake.
Brown mwenye umri wa miaka 25, ali-tweet kupitia ukurasa wake wa Twitter Jumanne(Feb.24) kuwa amekataliwa kuingia Canada na kwamba matamasha yake yaliyokuwa yafanyike katika miji ya Montreal na Toronto yamefutwa.
”Watu wangu wa Canada, serikali imenikatalia
kuingia. Nitarudi majira haya ya joto na natumaini nitawaona mashabiki
wangu wote wa Canada”, aliandika Chris Brown.
Msemaji wa Brown, Nicole Perna alithibitisha kuwa kitengo cha uhamiaji cha Canada kilimkatalia bosi wake kuingia nchini humo .
Alisema Brown anaweza kuomba kurudi katika siku za baadaye na anampango wa kufanya hivyo.
Nae Msemaji wa huduma za mipaka ya Canada, Stephane Malepart
amesema nchi yake imemzuia supastaa huyo kutokana na sababu kadhaa ikiwa
ni pamoja na kuhusika katika shughuli za uhalifu.
Hii sio mara ya kwanza kwa Chris Brown
kunyimwa kuingia katika nchi za watu, kwani mwaka 2010 msanii huyo
alikataliwa kuingia nchini uingereza na kulazimishwa kuzikosa shoo zake
nne.
Serikali ya Uingereza ilisema kwamba imemkatalia msanii huyo kwa sababu ya rekodi yake ya nyuma ya makosa ya jinai.
Mwaka jana ‘Brown’ alifungwa jela kwa takribani miezi 3 kwa
kukiuka majaribio yake baada ya kupatwa na hatia ya kushambulia nje ya
hoteli mjini Washington mwaka uliopita, kama hiyo haitoshi alikuwa
katika majaribio baada ya kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake Rihanna
kabla ya utolewaji wa tuzo za Grammy mwaka 2009.
Kwa picha rahisi utaweza kuona ni jinsi gani wingi wa matukio
hayo ya jinai yanavyomgharimu hitmaker huyo wa Loyal na kujikuta
akipishana na mkwanja mrefu.
Hili linaweza kutumika kama fundisho kwa wasanii wetu wa hapa
nyumbani kwamba too much Ego will kill your talen. Bad Lucky Bruh C.B.
USELA WAMPONZA CHRIS BROWN, AKATALIWA KUINGIA CANADA, ALAZIMIKA KUVUNJA MATAMASHA YAKE
Reviewed by crispaseve
on
02:08
Rating:

Post a Comment