BANDIKA BANDUA : EX WA NICKI MINAJ AJIWEKA KWA SUPASTAA HUYU MWINGINE WA KIKE

Minaj, Safaree Samuels na K.Michelle
Huenda ex wa Rapa Nicki Minaj, Safaree Samuels akawa na nyota
ya chips mayai au zali la ku-date na wanawake mastaa baada ya hivi
karibuni uji wa moto kutoka katika tovuti ya udaku ya TMZ kudakuza kuwa
sharobaro huyo yupo katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki
K.Michelle.
Kwa mujibu wa TMZ iliwafuma wawili hao wakiwa faragha eneo la
VIP katika klabu ya usiku ya Stage 48 iliyoko mjini New York nchini
marekani katika siku ya wapendanao yaani Valentine’s Day wakila ujana
sambamba na Safaree kumtumia zawadi ya maua mwanadafada huyo.
Safaree anatajwa kuwa karibu mno na K.michelle wakitajwa
kutumia muda mwingi wakiwa pamoja sehemu mbalimbali za bata, kupigiana
simu na kutumia meseji huku zilipendwa wake ‘Minaj’ akiwa mikononi mwa
Rapa Meek Mill na kujikuta wakiunda couple flani hivi amaizin iliyopewa
jina la Omeeka, .
Katika kupigia mstari ule msemo usemao, ”Ukisema wa nini??,
wenzako wanasema watampata lini??”, K.Michelle alipost video kupitia
ukurasa wake wa Instagram akitwerk juu ya biti ya nyimbo ya ex huyo wa
Minaj akionyeshe amekolea. Wacha muvi iendelee
BANDIKA BANDUA : EX WA NICKI MINAJ AJIWEKA KWA SUPASTAA HUYU MWINGINE WA KIKE
Reviewed by crispaseve
on
02:08
Rating:

Post a Comment