HAT-TRICK YA HISTORIA UNITED: SIKU KAMA YA LEO ‘DWIGHT YORKE’ ALIWEKA REKODI HII NDANI YA OLD TRAFFORD
Kwa
wale wapenzi na mashabiki nazi wa mashetani wekundu ‘Manchester United’
bila ya kupepesa watakuwa bado na kumbukumbu katika vichwa vyao ya
hat-trick iliyofungwa na mshambuliaji hatari wa enzi hizo ‘Dwight
Yorke’ mnamo Feb.25 mwaka 2001 ndani ya dakika 22 ambayo hadi leo haijavunjwa wakati United ilipomenyana na Arsenal.
Katika mchezo huo ulishuhudia Man United ikimaliza dakika 90
kwa kuwaadhibu washika mtutu hao wa jiji la London jumla ya magoli 6 -1
katika mtanange uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford huku mabao
mengine ya United yakipachikwa na Roy Keane, Ole Solskjaer na Teddy
Sheringham katika msimu wa 2000/01.
”Today is the anniversary of one of the most
memorable first halves at Old Trafford – Dwight Yorke’s hat-trick inside
22 minutes against the Gunners, during an eventual 6-1 win!
#classicmufc”, waliandika United katika ukurasa wao wa insta. Itazame Hat-Trick Hiyo hapo chini.
HAT-TRICK YA HISTORIA UNITED: SIKU KAMA YA LEO ‘DWIGHT YORKE’ ALIWEKA REKODI HII NDANI YA OLD TRAFFORD
Reviewed by crispaseve
on
02:03
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
02:03
Rating:


Post a Comment