Vijana wa Halmashauri za Kibondo na Kakonko waishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kibondo Bw. Fred EliyaSaphy (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Kitengo
cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.
Esther Riwa wakati alipowasili na ujumbe wake kutoka wizarani kwa ajili ya
shughuli za mafunzo kwa Vijana na ufuatiliaji wa miradi ya vikundi vya Vijana
wilayani hum oleo mjini Kibondo.

Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga(wa kwanza kulia) akielezea jambo kwa
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Bw. Fred EliyaSaphy
(katika) walipotembelea ofisini kwake leo kwa ajili ya kujitabulisha kabla ya
kuanza utekelezaji wa ziara yao wilayani humo. Kutoka kushotoni Kaimu Afisa
Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kibondo Bw. Abel Nuba na wapili kutoka kulia ni
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi. Esther Riwa
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibondo
Bw. Moshi Hussen (wa kwanza kushoto) akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa
Afisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina
Sanga(wa kwanza kulia) walipofika ofisini kwake leo kwa ajili ya kujitabulisha
kabla ya kuanza utekelezaji wa ziara yao wilayani humo. Kutoka kushoto kwa Kaimu
Katibu Tawala ni Afisa Vijana wa Wilaya
ya Kibondo Bi. Safi Mtula, Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa, Mkuu wa Kituo cha Vijana
Sasanda Mbeya Bw. Laurian Masele na Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya
Kibondo Bw. Abel Nuba .
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akiwasilisha
mada kuhusu stadi za masha kwa vijana wa Wilaya za Kibondo na Kakonko katika
mafunzo yaliyofanyika leo mjini Kibondo.

Afisa Vijana wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akiwasilisha mada kuhusu mwongozo
wa mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Wilayani Kibondo katika warsha
iliyoandalliwa na Wizara hiyo na kushirikisha jumla ya Vijana 83 kutoka katika
Halmashauri za Kibondo na Kakonko.

Baadhi ya Vijana kutoka Wilaya za
Kibondo na Kakonko wakifuatilia mada zilizokuwa zina wasilishwa na wataalamu
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hawapo pichani) wakati
wa mafunzo kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha,Uongozi Bora na
Sera ya Maendeleo ya Vijana leo wilayani Kibondo.
Picha na Frank Shija, WHVUM
Vijana wa Halmashauri za Kibondo na Kakonko waishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Reviewed by crispaseve
on
01:44
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
01:44
Rating:

Post a Comment