MZEE YUSSUF NA ISHA MASHAUZI WATHIBITISHA RASMI MTANANGE WA JAHAZI NA MASHAUZI CLASSIC
Hatimaye
wakurugenzi wa Mashauzi Classic na Jahazi Modern Taarab, wamefanya
mkutano na waandishi wa habari na kuthibitisha kuwepo kwa onyesho la
pamoja la makundi hayo yenye nguvu katika muziki wa taarab.
Onyesho
hilo litafanyika mwezi huu Jumapili tarehe 22 ndani ya ukumbi wa
Travertine Hotel Magomeni. Mkurugenzi wa Jahazi, Mzee Yussuf na
mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhan maarufu kama Isha
Mashauzi, wamesema siku hiyo hatumwi mtoto dukani.
Wakiongea
katika mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu jioni
katika hotel ya Travertine Hotel, wakurugenzi hao ambao wote ni waimbaji
nyota, wakasema onyesho hilo si mpambano lakini pia sio la masihara
kwani kila bendi imejipanga kuhakikisha inaangusha burudani iliyokwenda
shule.

Kutoka kushoto ni Meneja wa Mashauzi Classic Ismail Rashid, Isha Mashauzi, Mzee Yussuf na Seif Magwaru meneja wa Jahazi Modern Taarab.
MZEE YUSSUF NA ISHA MASHAUZI WATHIBITISHA RASMI MTANANGE WA JAHAZI NA MASHAUZI CLASSIC
Reviewed by crispaseve
on
07:49
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
07:49
Rating:

Post a Comment