Elimu ya uongozi bora yatolewa kwa viongozi wa vikundi vya vijana Kata ya Selela

Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa katikati akizungumza na Vijana wa Kata ya
Selela (hawapo pichani) wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za
Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Kata ya Selela Halmashauri
ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda
Mbeya Bw. Laurean Masele na kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara
hiyo Bi. Amina Sanga

Vijana wa Kata ya Selela wakisikiliza kwa makini
mada zilizokua zikitolewa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za
Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Kata ya Selela Halmashauri
ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.

Afisa Maendeleo ya
Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Mesha Singoyo akifafanua
jambo kwenye semina ya vijana wa Kata ya Selela kuhusu Ujasiriamali, Ujuzi na
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya
Monduli Mkoani Arusha

Afisa Maendeleo ya Vijana
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga (kulia)
akizungumza na wanakikundi cha Naisho wanaomiliki mradi wa kunenepesha ng’ombe
na kuziuza wakati wa kutembelea miradi ya vijana wa Kata ya Selela Halmashauri
ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Wapili kushoto ni mhamasishaji kutoka
Wizara hiyo Bibi. Ester Riwa na wanne kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana
Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.

Baadhi ya ng’ombe zinazomilikiwa na vijana wa
Naisho Group zikiwa machungani katika kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya
Monduli Mkoani Arusha.

Mkuu wa Kituo cha
Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele (wapili kulia) akifafanua jambo walipotembelea
mradi wa kikundi cha Songambele kinachojishughulisha na kilimo katika Kata ya Selela
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Kulia ni mhamasishaji kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa.

Moja ya shamba la
mahindi linalomilikiwa na kikundi cha Songambele katika kata ya Selela
Halmashauri ya Wilaya ya Mondili Mkoani Arusha. Picha
na: Genofeva Matemu – Maelezo, Monduli
Elimu ya uongozi bora yatolewa kwa viongozi wa vikundi vya vijana Kata ya Selela
Reviewed by crispaseve
on
02:41
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
02:41
Rating:

Post a Comment