WANAZUONI WAJADILI MUSTAKABALI WA TANZANIA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI
Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.
Mkurugenzi wa Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP,
Philippe Poinsot akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya
siasa na kiraia katika mkutano huo.
Aidha
alisisitiza kwamba demokrasia sio suala jepesi, lakini watanzania
wanastahili kujivuna kwa hatuha waliyofikia katika mambo mbalimbali
ambayo hata mataifa mengine ya Ulaya hayajafikia.
Alisema
mwaka 1994 wakati taifa linaingia katika vyama vingi taifa lilikuwa na
vyama 13 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 1995 lakini sasa tunapozungumza
kuna vyama 22 vyenye usajili wa kudumu, wigo wa kuwania dola ukiwa
umetanuka zaidi.
Pia
alisema mafanikio mengine ni namna ambavyo vyombo vya habari vina
nafasi kubwa ya kuandika inavyoona sawa, japo kumekuwa na tukio la
kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi, Mtanzania na Mwananchi, lakini
kadhia hizo haziondoi ukweli kuwa kumekuwepo na uhuru mkubwa wa vyombo
vya habari.
Dk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.
Alisema
taifa hili halina sababu ya kuomba radhi kwa mafanikio yaliyopo na
changamoto zake katika siasa kwani uelewa katika masuala ya siasa
unazidi kutanuka.
Alisema
pamoja na mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na
utamaduni wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na
aidolojia (itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa
ya siasa na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.
Alisema
kutanuka kwa wigo wa ushiriki wa kuwania dola (vyama vingi vya siasa)
kunatakiwa kwenda sanjari na kujenga utamaduni huo wa kuimarisha ustawi
wa utamaduni wa vyama vingi.
WANAZUONI WAJADILI MUSTAKABALI WA TANZANIA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI
Reviewed by crispaseve
on
02:30
Rating:

Post a Comment