UZINDUZI WA KITABU CHA KUJIFUNZA KILINGALA CHA TSHIMANGA KALALA ASSOSA NA KAVASHA CLUB…
Jumapili
hii tarehe 03-May-2015, mwanamuziki mkongwe Tshimanga Kalala Assosa
atazindua kitabu kilichokuwa kikisubiriwa na watu wengi sana kwa muda
mrefu mno.
Ni kitabu cha “kuJifunza LINGALA kwa Kiswahili”.
Uzinduzi huo utaambatana na tukio kubwa sana la wana Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni cha pamoja (dinner).
Ni
ndani ya ukumbi wa MRC Jumapili (03-May-2015) kuanzia saa 12 hadi saa 3
jioni. MRC ndio ukumbi ambao “Club Raha Leo Show” ya TBC1 ilikuwa
inafanyikia.
Tshimanga
Kalala Assosa amepata kupiga bendi nyingi kubwa hapa Afrika kama
Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie), Orchestre Lipua Lipua,
Orchestre Les Kamale (akiwa na Nyboma, Mulembu na Kizunga) pamoja na
Fukafuka zote za Congo DRC. Kwa hapa Tanzania amefanya kazi na Mlimani
Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre Makassy, Orchestre Mambo
Bado, Legho Stars na Bana Maquis.
Mgeni rasmi wa tukio atatangazwa.
Wote mnakaribishwa. Wahi bila kukosa. Kiingilio ni BURE.
UZINDUZI WA KITABU CHA KUJIFUNZA KILINGALA CHA TSHIMANGA KALALA ASSOSA NA KAVASHA CLUB…
Reviewed by crispaseve
on
04:26
Rating:

Post a Comment