UZINDUZI WA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA SHINYANGA
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga akiagana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bwana
Michael Mhando na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri wa KItaalamu
Dokta Frank Lekey baada ya uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa.
Akizungumza
kuhusu mpango huo wa kupeleka madaktari bingwa katika mikoa ya
pembezoni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bwana Michael Mhando amesema
Mfuko unatekeleza mpango huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za
kupeleka huduma bora za matibabu kwa wananchi wote.
Ameongeza
kuwa utekelezaji wa mpango huo unakusudia kuwapunguzia wananchi wamikoa
ya pembezoni gharama za kufuata huduma hizo katika hospitali kubwa
ambazo ziko mbali na maeneo wanayoishi.
Hadi
sasa mpango huo umeshatekelezwa katika mikoa ya Lindi, Kigoma, Rukwa,
Katavi, Pwani, Tabora, Mara Manyara na Mtwara na kuwanufaisha zaidi ya
wananchi 7800.
Katiba
hotuba yake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amewapongeza madaktari bingwa
hao kwa moyo wao wa kujitolea na kuwataka wengine kuiga mfano wao. Aidha
amemwagiza Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa vifaa
tiba vilivyotolewa na NHIF viendelee kutunzwa ili viwanufaishe wananchi
wengi zaidi.
Bwan
Rufunga pia amewahimiza wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujiunga kwa
wingi katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waondokane na unyonge wa
kutibiwa kwa kutumiwa fedha taslimu na badala yake watibiwe kwa kutumia
kadi za CHF.
UZINDUZI WA HUDUMA ZA MADAKTARI BINGWA SHINYANGA
Reviewed by crispaseve
on
06:57
Rating:
Post a Comment