WASANII WAOMBA KUPUNGUZIWA KODI KWENYE VIFAA VYA MUZIKI.
1 Msanii
G Nako kutoka Kundi la muziki wa kizazi kipya la Weusi akiimba sambamba na
msanii mchanga ambaye hakufahamika mara moja kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA
mapema wiki hii.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya kutoka Kundi la Weusi Nick wa Pili (Kushoto)
akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani)
kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayofanyika kwa mwezi mara mbili
siku ya Jumatatu makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala
Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto kwake ni wasanii
wanaounda kundi hilo John Simon aka Joh Makini na G Nako na Afisa kutoka
BASATA Bi. Elineca Ndowo.
1 Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Mitaji na Misaada kwa wasanii kutoka Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) Bi. Elineca Ndowo (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako
pichani) kuhusu masuala mbalimbali kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ambayo
huandaliwa kwa mwezi mara mbili ziku ya Jumatatu na Baraza hilo. Wengine katika
picha kulia kwake ni Wasanii G Nako na John Simon maarufu kama Joh Makini
wanaounda kundi la muziki wa kizazi kipya la Weusi.
Baadhi
ya wasanii nchini wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Fedha kufikiria
kupunguza au kufuta kabisa ushuru wa forodha unaotozwa kwenye vifaa vya
muziki wanavyoagiza kutoka nje ili kukuza Sanaa na kusaidia mamilioni ya
vijana ambao wamejiajiri kupitia sekta hiyo.
Akizungumza
kwa niaba ya wasanii mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) mmoja wa wasanii anayeunda kundi la muziki wa
kizazi kipya la Weusi Nick wa Pili alisema kwamba, kwa sasa sekta hiyo
ni kimbilio la ajira kwa vijana wengi kwa hiyo Serikali haina budi
kupunguza kodi kwa zana mbalimbali zinazotumiwa na wasanii ili
kurahisisha uzalishaji, kukuza tija na uchumi.
“Wasanii
wengi kwa sasa wanakwenda kufanya video na kutengeneza muziki nje ya
nchi. Hii inatokana na teknolojia yetu kuwa chini ya wenzetu. Naamini
Serikali ikipunguza kodi katika vifaa hivi na kuwawezesha wataalam
tulionao basi nchi zote jirani zitakimbilia kwetu” alisema Nick.
Aliongeza kwamba
vipaji vya wasanii vipo vingi lakini kutokana na uzalishaji duni wa kazi za
muziki na hata filamu wasanii wamejikuta wakishindwa kushindana ipasavyo nje ya
nchi na mara nyingi kutumia gharama kubwa katika kufuata teknolojia hizo za juu
nchi za nje na hivyo kuikosesha serikali mapato.
“Wasanii wanakwenda
kulipa zaidi ya milioni arobaini kwa video moja tu nje ya nchi, hizi fedha
zinakwenda kukuza uchumi wa nchi zingine. Naamini kama Serikali ikijenga
mazingira mazuri ya kiteknolojia na zaidi kushusha gharama hizi basi nchi yetu
itafaidika zaidi na Sanaa” alizidi kusisitiza Nick.
Kwa upande wake
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mitaji na Misaada kwa wasanii kutoka BASATA Bi.
Elineca Ndowo alisema kwamba sekta ya Sanaa nchini inazidi kukua na hivyo
lazima wasanii nao wafikirie kufanya kazi kisasa na kwa kufuata taratibu zote
ili kuipa serikali uhakika katika kupanga kulingana na hali halisi.
“Sekta ya Sanaa
inakua, lazima tuisaidie Serikali kuipa takwimu sahihi na moja ya njia ya
kuhakikisha hili ni kwa wasanii kujisajili, kusajili kazi zao na kuhakikisha
taarifa sahihi na kwa wakati zinapatikana. Hili litarahisisha upangaji wa
mipango” alisema Bi. Ndowo.
WASANII WAOMBA KUPUNGUZIWA KODI KWENYE VIFAA VYA MUZIKI.
Reviewed by crispaseve
on
07:06
Rating:
Post a Comment