NI DKT JOHN POMBE MAGUFULI KUIPEPERUSHA BENDERA YA CCM KITI CHA URAIS,AIBUKA NA ASILIMIA 87.1 YA KURA.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ndie Mgombea Urais wa Tanzania.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana na Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, mchana huu hapa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre, Mjini Dodoma. Dkt. Magufuli ameibuka kidedea kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake Amina Salum Ally, akiibuka na kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro, akipata kura 59. Viongozi wakuu wameenda kwenye kikao hivi sasa cha kujua nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Urais. hivyo tutaendelea kuwajuza zaidi, endelea kuwa jirani na Libeneke lako pendwa la Globu ya Jamii.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza wake, Mh. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumtangaza, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre, Mjini Dodoma mchana huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mgombea Mwenza wake, Mh. Samia Suluhu Hassan wakati akimtambuliasha kwa wanaCCM na Watanzania.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mh. Samia Suluhu Hassan akipombewa na Spika wa Bunge, Mh. Anne Makinda pamoja na viongozi wengine. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda.
Ama
kwa hakika hayawi hayawi sasa yamekuwa,Mchakato wa kumpata mgombea
Urais ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) umefanyika hatua kwa hatua na
hatimaye kapatikana atakaipeperusha bendera ya CCM katika kiti cha Urais
kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo baadae mwaka huu.
Ni
John Pombe Magufuli ambaye baada ya Wajumbe wa Mkutano mkuu wa chama
hicho kupiga kura kwa wagombea Urais Watatu ambao ni Dkt John Pombe
Magufuli ,Dkt Asha Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ali.
Kura
zilipigwa jana katika Mkutano mkuu wa chama hicho ndani ya ukumbi wa
Convetion Center mjini Dodoma,na matokeo yake yametangazwa rasmi mapema
leo asubuhi kuwa jumla ya kura zilizokuwa zimepigwa zilikuwa 2422,kura
zilizoharibika zilikuwa 6 na kula halali zilipatikana 2416.
Katika
kinyang'anyiro hicho Dkt Asha Rose Migiro alipata kura 59 ambayo ni
2%,Dkt John Pombe Magufuli alipata kura 2104 ambayo ni 87.1 % na Balozi
Amina Salum Ali aliyepata kura 255 ambayo ni asilimia 10.5.
Kwa matokeo hayo,imetangazwa rasmi kuwa Dkt John Pombe Magufuli ndiye atakaibeba bendera ya CCM katika kuwania kiti cha Urais
Kwa matokeo hayo,imetangazwa rasmi kuwa Dkt John Pombe Magufuli ndiye atakaibeba bendera ya CCM katika kuwania kiti cha Urais
NI DKT JOHN POMBE MAGUFULI KUIPEPERUSHA BENDERA YA CCM KITI CHA URAIS,AIBUKA NA ASILIMIA 87.1 YA KURA.
Reviewed by crispaseve
on
06:07
Rating:
Post a Comment