Header AD

MWENGE WA UHURU WAANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI RUKWA LEO

Mkuu wa Wilaya ya Momba Richard Mbeho kushoto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya leo tarehe 11 Julai 2015 tayari kwa kuanza mbio zake za siku nne Mkoani Rukwa. Mwenge wa Uhuru utatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni 11. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akishika Mwenge wa Uhuru ulipowasili  Mkoani Rukwa leo tarehe 11 Julai 2015.

 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mkutano Mkoani Rukwa wakiwa wamebeba bendera ya taifa kwa ajili ya kuipeleka na kuipeperusha eneo la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Mbeya kwenda Mkoa wa Rukwa.
 Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akishika mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili Mkoani Rukwa leo.
MWENGE WA UHURU WAANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI RUKWA LEO MWENGE WA UHURU WAANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI RUKWA LEO Reviewed by crispaseve on 05:56 Rating: 5

No comments

Post AD