SPORTS XTRA NDONDO CUP YAZINDULIWA RASMI, ABAJALO, FC KAUZU MUZIKI WAO..OGOPA SANA!
Baada ya kuisubiri kwa muda mrefu burudani hii adimu! Sasa utamu umewadia!!
Msimu
wa pili wa mashindano ya Sports Xtra Ndondo Cup chini ya udhamini wa
Dr. Mwaka, Daktari bingwa wa masuala ya Afya ya uzazi na Tiba asilia
kutoka kituo cha Foreplan Clinic, kilichopo Bungoni, Ilala, Dar es
salaam umezinduliwa rasmi katika uwanja wa Bandari, Tandika, jijini Dar
es salaam.
Mechi
ya ufunguzi yenye mvuto wa aina yake imepigwa jana ikiwakutanisha
mabingwa watetezi, Abajalo FC ya Sinza Dar es salaam dhidi ya timu
iliyojizolea Umaarufu ya wauza mitumba wa Tandika, FC Kauzu na hadi
dakika 90 zinamalizika wanaume hao wa ‘Shoka’ walitoka suluhu (0-0).
Sports
Xtra Ndondo Cup ni mashindano yenye heshima kubwa kwa sasa na kwa
kulitambulia hilo, Mgeni rasmi alialikwa kufungua pazia ambaye ni Mjumbe
wa kamati ya Utendaji ya TFF anayewakilisha mkoa wa Dar es salaam,
Wilfred Kidau akiambatana na mwenyekiti wa chama cha soka cha Dar es
salaam (DRFA), Almas Kasongo pamoja na mwenyekiti wa chama cha soka
wilaya ya Temeke (TEFA), Peter Muhinzi.
Kwa
wale ambao hawakushuhudia!, hakika mechi ya ufunguzi ilikuwa nzuri mno
ikichagizwa na wachezaji wa ligi kuu wanaokipiga katika michuano hayo,
mfano FC Kauzu walimtumia mshambuliaji hatari wa Kagera Sugar, Atupele
Green na ngome ya ulinzi iliongozwa na beki wa Mbeya City, Juma Said
Nyosso.
Cha
kufurahisha! FC Kauzu wanatumia jezi za Zambarao kama ilivyo kwa Mbeya
City FC, hivyo Nyosso alionekana kama anakipiga katika kikosi hicho cha
Juma Mwambusi. Abajalo FC wao walikuwa na mtu kama Paul Maona na nahodha
wao George Kavila wanaokipiga Kagera.
Mashabiki
zaidi ya Elfu tano walihudhuria mechi hiyo iliyojaa vitimbwi, mbembwe
za kila aina na nimekuwekea baadhi ya picha zikionesha shamrashamra za
mashabiki wa Sports Xtra Ndondo Cup Chini ya udhamini wa Dr. Mwaka.
SPORTS XTRA NDONDO CUP YAZINDULIWA RASMI, ABAJALO, FC KAUZU MUZIKI WAO..OGOPA SANA!
Reviewed by crispaseve
on
05:54
Rating:
Post a Comment