MAANDAMANO YA AMANI YA WADAU WA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YAFANYIKA LEO JIJINI DAR
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IMEELEZWA kuwa nchi zilizoendelea ndio zinaongoza katika
uharibifu wa mazingira kwa utumiaji wa Nuklia ,pamoja na uchimbaji wa Chuma hivyo
zinawajibu kuwekeza katika mabadiliko tabia nchi kutokana na kuchangia hali
hiyo .
Hayo ameyasema leo Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia
Nchi Tanzania (CAN),Sixbaty Mwanga wakati wa matembezi ya amani ya Mabadiliko
ya Tabia ya Nchi yaliyofanyika viwanja vya
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Amesema mabadiliko ya tabia ya nchi yamezidi kukua kwa kasi
kutokana na uharibuifu wa mzingira unaofanywa na binadamu kwa shughuli za kila
siku huku jitihada za kukabili
mabadiliko hayo zikichukua asilimia ndogo.
Mwanga amesema malengo 17 ya maendeleo endelevu ya tabia ya nchi
ya mwaka 2015 -2030 kunahitaji viongozi kushughulikia katika
vyanzo mbalimbali vya fedha katika kuweza kufikia malengo na kushindwa kufanya hivyo kutakuwa na madhara
ya ukame,njaa, vifo pamoja na mafuriko.
Aidha amesema kuna mikutano mbalimbali inakuja hivyo ni kila
mtu kwa nafasi yake ashiriki katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi
katika nchi iweze kuwa na uchumi imara.
Wadau wa mabadiliko ya tabia ya nchi wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegeme
wakihamasisha urtunzaji wa mazingira katika maandamano ya amani ya
kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu
cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam leo.
Wanafunzi
wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee ya jijini Dar es Salaam wakiwa
na mabango mbalimbali yenye jumbe tofautitofauti ili kuhamasisha yamii
kuachana na uchafuzi wa mazingira ili kuokoa maisha ya watanzania
kutokana na kuwa na majamba mbalimbali yanayosababishwa na mabadiliko ya
tabia ya nchi, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi
yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu
cha Dar es Salaam leo.
Wanafunzi
wa shule ya Sekondari ya JKT Jitegemee wakiimba wimbo unaohamasisha
utunzaji wa mazingira ili kuepukana na uchafunzi wa mazingira kwa njia
mbalimbali, katika maandamano ya amani ya kupiga vita mabadiliko ya tabia ya nchi
yaliyofanyika kuanzia Chuo kikuu cha Ardhi mpaka viwanja vya chuo kikuu
cha Dar es Salaam leo.
MAANDAMANO YA AMANI YA WADAU WA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YAFANYIKA LEO JIJINI DAR
Reviewed by crispaseve
on
05:53
Rating:
Post a Comment