WANAWAKE WATAKIWA KUJIAMINI KATIKA NAFAZI ZAO ZA UONGOZI -KAIRUKI
Nabu
waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki
akizungumza na wanawake katika mkutano wa kuwajengea uwezo wanawake
katika masuala ya uongozi uliofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar
es Salaam.
Katibu
mtendaji wa uongozi institue,Profesa Joseph Semboja akizungumza katika
mkutano wa kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya uongozi
uliofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wanawake walioshiriki mkutano wa kuwajengea uwezo katika masuala ya
uongozi uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wanawake walioshiriki mkutano wa kuwajengea uwezo katika masuala ya
uongozi uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
NAIBU Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki amewataka
wanawake kujiamini katika nafasi za uongozi wanazozipata katika kuweza
kufikia asilimia ya 50 kwa 50.
Hayo
aliyasema katika mkutano wa wanawake ulioandaliwa na uongozi
Instute,Kairuki amesema katika kuelekea katika uchaguzi mkuu wanawake
wajitokeze katika nafasi mbalimbali ili kuweza kubadilika.
Amesema
katika ngazi mbalimbali za maamuzi katika bodi zilizopo nchini ni idadi
ndogo za wanawake ikilinganishwa na wanaume hali ambayo sasa inatakiwa
kuweka kupaumbele katika bodi kuwa na uwakilishi wa wanawake.
Kairuki
amesema sasa ni wakati wa mabadliko kwa wanawake kuonyesha uwezo katika
kazi mbalimbali na kujenga mazingira ya kujiamini katika kazi
iwe nafasi za ukurugenzi na kazi nyinginezo za serikali na sekta
binafsi.
Nae
Katibu Mtendaji wa Uongozi Institute,Profesa Joseph Semboja amesema
wameanza program hiyo katika kuwainua wanawake katika nafasi za uongozi
katika kuweza kufikia malengo ya asilimia 50 kwa 50.
Sembomja
amesema wanawake katika kuelekea uchaguzi mkuu ni fursa kwao kujitokeza
kutokana na mafunzo mbalimbali wanayopata kutoka kwa wanawake
waliokatika nafazi za uongozi.
WANAWAKE WATAKIWA KUJIAMINI KATIKA NAFAZI ZAO ZA UONGOZI -KAIRUKI
Reviewed by crispaseve
on
07:31
Rating:
Post a Comment