BODI YA FILAMU YASITISHA USAMBAZAJI WA “IMEBUMA”
Mhusika
Mkuu katika filamu ya “Imebuma” Bw. Eliasa Mkaly (Rashidi kisoda)
akimbembeleza muigizaji na mtayarishaji wa filamu hiyo Bi Sarah Nyika
(Asha Mauno) mara baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kusitizaji usambazaji
wa filamu hiyo.( Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO).
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso akizungumza na
waigizaji wa filamu ya “Imebuma” (Hawapo Pichani) wakati wa ukaguzi wa
filamu hiyo kabla ya kupelekwa sokoni kulia ni 2 Afisa Utamaduni Bw.
Julius Tairo.
Afisa
Utamaduni Bw. Julius Tairo (wa Pili Kushoto) akitoa maelekezo kwa
waigizaji wa filamu ya “Imebuma” (Hawapo Pichani) wakati wa ukaguzi wa
filamu hiyo kabla ya kupelekwa sokoni kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi
ya Filamu Tanzania Joyce Fisso.
Mhusika
Mkuu katika filamu ya “Imebuma” Bw. Eliasa Mkaly (Rashidi kisoda)
akitoa maelezo kuhusu filamu hiyo wakati wa ukaguzi wa filamu ya
“Imebuma” kabla ya kupelekwa sokoni kulia ni waigizaji wa filamu hiyo.(
Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM)
Na Shamimu Nyaki WHUSM
Bodi ya Filamu Tanzania imesitisha usambazaji wa filamu ya “Imebuma” mpaka pale maudhui yake yatakapofanyiwa marekebisho.
Akisitisha
usambazaji wa filamu hiyo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania
Bi Joyce Fisso amesema mtengenezaji wa filamu hiyo hana kibali cha
kutengenza filamu kutoka Bodi ya Filamu na hajazingatia Sheria na kanuni
za utengenezaji wa filamu.
Bi Joyce
Fisso amesema filamu hiyo imesitishwa kwenda sokoni kutokana na kukiuka
vifungu vya kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka
2011 ambayo inakataza kuonesha namna yoyote ya udhalilishaji wa
kibinadamu katika filamu na maigizo.
“Baada ya
kuangalia kwa makini filamu hii na kuona mapungufu ambayo yanakinzana
na Kanuni za Sheria ya filamu na Michezo ya kuigiza nimeamua kuisitisha
usambazaji wake mpaka pale wahusika watakaporekebisha maudhi yake”
Alisema Bi Joyce.
Bi Joyce
amefafanua kuwa filamu hiyo imeonesha baadhi ya matukio ya udhalilishaji
wa kibinadamu, ushawishi wa matendo ya ngono na ushoga ambayo ni
kinyume na madili ya mtanzania.
Aidha kwa
upande wake Afisa Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Julius
Tairo amewataka waandaaji na waigizaji wa filamu nchini kufanya utafiti
wa kutosha kuhusu maudhui ya filamu kabla ya kutengeneza ili kuondokana
na utengenezaji wa filamu zisizofata Sheria na kanuni za utengenezaji
wa filamu Tanzania.
BODI YA FILAMU YASITISHA USAMBAZAJI WA “IMEBUMA”
Reviewed by crispaseve
on
07:15
Rating:
Post a Comment