Header AD

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBARA AKABIDHI VIFAA ZAHANATI YA KIMARA

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi, akimkabidhi vifaa vya huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dkt. Alphoncina Mbinda, wakati wa hafla maalum iliyofanyika jana, kwenye Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 5.1, vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi wa Jumuia ya Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya Kinondoni, Stanley Mkandawile, (wapili kulia), na katikati ya Makamu na Mganga Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk.
 Wana-CCM Kata ya Kimara wakishangilia wakati wa hafla hiyo.
 Wana-CCM na wananchi wakisebeneka kucheza muziki wa taarab, kushangilia makabidhiano ya vifaa hivyo vya huduma na tiba kwa Zahanati yao.
Baadhi ya wanachama wa Jumuia ya Wazazi waliohudhuria sherehe hiyo. Picha na Bashir Nkoromo
Reviewed by crispaseve on 08:22 Rating: 5

No comments

Post AD