Header AD

MISS UTALII MKOA WA KAGERA NI IRENE BWIRE

MISS UTALII KAGERA 2012 MISS IRENE BWIRE KATIKATI NA MSHINDI
WA PILI MISS JANIA ABDUL KUSHOTO NA MISS MAYOR KASHUMBA MSHINDI WA
TATU KULIA.

Mrembo Irene Bwire, mwishoni mwa wiki ameibuka mshindi wa Taji la Miss Utalii Kagera 2012, katika shindano lililofanyika katika ukumbi wa Rinas Club mjini Bukoba mkoani kagera siku ya jumamosi tarehe 14-7-2012. Irene alitwaa taji hilo kwa kuwashinda warembo wengine 14, katika shindano ambalo mkuu wa Wilaya ya Bukoba mama Pangani alikuwa mgeni rasmi. Mrembo Jania Abdul alikuwa mshindi wa pili na Mayor Kashumba alikuwa mshindi wa tatu, hivyo wote pamoja na mshindi wa nne,watano na mshindi wa taji la Miss Utalii Vipaji watawakilisha mkoa wa kagera katika fainali za Miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya Magharibi,zitakazo fanyika mkoani Mara mwezi Oktoba 2012.

Katika shindano hilo ambalo lilisindikizwa na burudani za muziki wa  asili na wa kizazi kipya ikiwemo bendi ya Diamond Sound pamoja na msanii BK Sanday  na makundi ya ngoma za asili za mkoa wa kagera, shindano hilo liliandaliwa na Dinner Fashion,huku Miss Utalii Kilimanjaro 2012 Evamary Gamba akiwa ni mwalimu wa warembo.


Mgeni rasmi , mkuu wa wilaya ya Bukoba aliwapongeza waandaaji kwa kufanikiwa kuaandaa shindano hilo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa ni kichocheo cha kutangaza utalii na utamaduni wa mkoa wa Kagera. Aidha alisema kuwa serikali na mkoa wa Kagera wanathamini sana mchango wa shindano hilo katika kuhamasisha na kutangaza utalii na utamaduni wa Tanzania pia mianya ya uwekezaji, na kuwataka wadau mbalimbali kuliunga mkono kwa kudhamini shindano hilo kila linapofanyika
Reviewed by crispaseve on 04:05 Rating: 5

No comments

Post AD