Header AD

Mkutano wa Kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi unaoendelea mjini Bangkok

 Mkurugenzi msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,Bw. Richard Muyungi, akifuatilia kwa makini mjadala unaeendelea katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi unaoendelea mjini Bangkok.
 Katikati ni Afisa mwanasheria kutoka ofisi ya makamu wa Rais Bi Margareth Meela, akifuatilia majadiliano ya masuala ya mkataba wa Kyoto (KP) katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi unaoendela mjini Bangkok. kushoto kwake ni muwakilishi kutoka Uingereza na kulia kwake ni muwakilishi kutoka Nchini marekani .

NA Evelyn Mkokoi, BANGKOK
Mkutano wa mwisho wa maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa 18 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu huko Doha Qatar, umeanza leo hapa mjini Bangkok, Thailand.

Mkutano huu unahusisha nchi zote wanachama kwa ngazi ya watalaamu, ili kukubaliana masuala yote ambayo yatahitaji kuamriwa na mawaziri au wakuu wan chi huko Doha. Masuala muhimu yanayojadiliwa ni pamoja na; makubaliano kuhusu jinsi ya kushiirkisha nchi zote duniani kupunguza uzalishaji wa gesi joto zinazosabisha kungezeka kwa joto la dunia.

 Kwa sasa joto la dunia limeongezeka kwa nyuzi joto zipatazo 0.8  kwa takriban miaka mia moja iliyopita, na kwa kuwa sasa gesijoto zinaongezeka sana inasadikiwa kuwa joto linaweza kuongezeka zaidi ya nyuzi joto mbili  kwa miaka hamsini ijayo kama nchi, hasa zile zilizoendelea,  hazitafanya juhudi za makusudi za kupunguza uzalishaji wa gesitoto.

 Majadiliano haya yanaonekana kuwa magumu kwa sababu, upunguzaji wa gesijoto unagusa uchumi  wa  nchi zilizoendea hasa katika sekta za viwanda, nishati na usafirishaji; sekta ambazo zinazalisha gesi hizi kwa wingi, Pamoja na hayo,  Mkutano huu utazungumzia na kukubaliana pia  kuhusu  mambo mbali mbali yaliyobaki kama kiporo katika mkutano wa Bonn ikiwa ni pamoja na masuala ya misitu, jinsi ya kuongeza juhudi za kukabilana na athari za mabadiliko ya tabinachi na upatikanaji wa fedha kukabilana na athari hizi. 

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huu, Bwana Richard Muyungi, Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais,  ambyae ni Mwenyekiti   wa Kamati  ya Dunia ya Sayansi na Teknologia ya Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi na pia Makamu wa Rais wa Mkataba akiiwakilisha Afrika, alisema Afrika ikiwa ni pamoja na nchi kama Tanzania  ina matumani makubwa kuwa nchi zote dunaini na hasa zilizoendelea ya kufanya juhudi za makusudi  za kupunguza gesijoto ili dunia iwe salama.

Pamoja na juhudi hizi alisistiza haja ya  kuzisaidia nchi ambazo tayari zinakabiliwa na athari kubwa kupewa msaada wa fedha na utaalamu kukabiliana na athari hizi. Alisema,msaada huu usiwe mkopo kwani ni wajibu wanchi ambazo zimesababisha tatatizo hili kulinda haki ya kuishi na kuwa na maendeleo yanayotakiwa kwa nchi nyingi za Afrika amabazo hazikusababisha tatatizo hili lakini zina uwezo mdogo wa kiuchumi kukabiloana na madhara haya makubwa, kitolea mfano wa athari mbali mbalia ambazo tayari zimejitokeza Tanzania, ikiwa ni pamoja na madhara makubwa yanayosababishwa kuongezeka kwa kina cha bahari kwa maeneo ya pwani mwa Tanzania na Zanzibar. 

Akiongea kwa kofia ya Makamu wa Rais kwa niamba ya Afrika, ameongeza kuwa, suala la matumizi ya nishati ya mafuta  kwenye sekta ya viwanda, usafiri na usafirishaji litabakia kuwa muhimu hadi nchi nyingi zinazoendeea hasa za Afrika zitakaposaidiwa kupata nishati mbadala, zitakazokuwa endelevu na kwa bei nafuu. Pamoja na nia njema ya nchi hizi   kutaka  kushirikiana katika kupunguza gesijoto, uchumi wanchi nyingi maskini utaendelea kutegemea nishati ya mafuta na makaa ya mawe kwani ndiyo inayoweza kupatika  kwa urahisi zaidi katika kujiletea maendelo endelevu kwa sasa.

Wakati huo huo, akifungua Mkutano huu, Mkurugenzi Mkuu wa ‘Secretariat’ ya Mkataba huu, Bi Christiana Figueres, alihimiza   nchi zote zilikubali kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na uwazi katika kukabilana na tatatizo hili ,  na mataifa yote yatambue  umuhimu wa kuhakikisha  upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoedelea katika kuhimili na  kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

 Aidha nchi nyingi zilizoendelea zilizozungumza zilisistiza haja ya kuheshimu Makubaliano yaliyo katika mkataba na hasa misingi muhimu iliyowekwa  kwa kutambua kuwa kuna nchi zenye wajibu wa msingi wa kutataz tatizo hili.

Ujumbe wa Tanzania unaowakilisha katika mkutano huu, unashirkisha pia Wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, na wataalamu wengine kutoka Ofsis ya makamu wa Rais mazingira.
Reviewed by crispaseve on 09:32 Rating: 5

No comments

Post AD