Header AD

BABYLOVE KALALA ANYAKUA TAJI LA REDDS MISS TANZANIA TALENT SHOW USIKU HUU

Mkurugenzi wa Miss TanzaniaBw. Hashim Lundenga akifungua rasmi shindano la Miss Tanzania Talent Show usiku huu  kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View iliyoko kandokando ya bahari yaHindi jijini Dar es salaam, warembo wameonyesha vipaji vyao mbele ya watazamaji na wapenzi wa masuala ya urembo na usiku huu watapatikana watano watakaonigia kwenye ano bora na kutangazwa rasmi kwenye shindano la Miss Tanzania litakalofanyika Ubungo Novemba 3 mwaka huu , katika picha katikati ni Mbunge wa Arusha mjini viti maalum CCM Catherin Magige na kulia ni  Mkurugeni wa Hoteli ya Girrafe Ocean View Bwana Charles Bekon.
Fullshangwe inakumuvuzishia moja kwa moja matukio yanayoendelea kwenye show hii ya Miss Tanzania Talent Show kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View  jijini Dar es salaam.
 
Mshindi wa Miss Tanzania Talent Show Babylove Kalala akicheza na nyika wakati wa shindano hilo lililofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View kandokando ya bahari ya hindi jijini Dar es salaam usiku huu.
Hawa  niyo walioingia tano bora ya shindano hilo lililofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Gorrafe Ocean View jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Hoteli ya Girrafe Ocean View Bwana Charles Bekon akikaribisha wageni mbalimbali waliofika katika shindano hilo.
Miss World Tanzania Lisa Jensen kulia akiongoza majaji wa shindano hilo usiku huu kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View usiku huu.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika show hiyo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyojiri ukumbini hapo usiku huu mdau, mdau chini ni matukio mbalimbali ya show hiyo jionee mwenyewe mambo yaliyojiri kwenye hoteli hiyo usiku huu ni burudani na kushangweka kwa kwenda mbele kutoka kushoto ni Fredy, David na Isack.

Reviewed by crispaseve on 02:49 Rating: 5

No comments

Post AD