Mke wa Waziri Mkuu
Mana Tunu Pinda akitoa hotuba ya kufungua Maonyesho ya Wanawake
Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es
Salaam ambapo amewahimiza wajasiriamali kujiunga katika ushirika ili
iwe rahisi kusaidiwa kupata mikopo, kutafuta masoko, kupanga bei nzuri
ya bidhaa zetu, kupata utaalam na teknolojia mpya. Kauli Mbiu ya ya
Maonyesho hayo mwaka huu ni “Msichana Amka, Ujasiriamali ni Ajira”.
Mama Tunu Pinda
akikata utepe kuzindua Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi wa Maendeleo ya
Wanawake Wajasiriamali (WEDEE) Ulio chini ya Shirika la Kazi Duniani
(WEDEE) wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Wanawake wajasiriamali ya
MOWE yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mama Pinda akipokea vitabu toka kwa Noreen Toroka (wa pili kulia) na Hopolang Phororo wa ILO.
Mama Tunu Pinda
akisoma kwa furaha kitini cha mafunzo ya Wajasiriamali baada ya
kufungua Maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Hopolang Phororo na
Noreen Toroka kutoka ILO.
Pichani Juu na Chini ni Mama Tunu Pinda akikagua baadhi ya mabanda na kujionea bidhaa mbalimbali katika maonyesho hayo.
Mama Tunu Pinda
akipokea kipeperushi kutoka kwa Noreen Toroka wa ILO walioandaa
maonyesho ya MOWE kwa kushirikiana na Taasisi ya Wanawake na Maendele0
(WAMA) iliyochini ya Mama Salma Kikwete.
Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja baada ya kufungua maonyesho ya MOWE 2012.
Reviewed by crispaseve
on
08:59
Rating:
Post a Comment