Header AD

BANK OF AFRICA TANZANIA SASA KUSHIRIKIANA NA AIRTEL TANZANIA KATIKA KUTOA HUDUMA YA AIRTEL MONEY NA UTOAJI MIKOPO KWA WASAMBAZAJI WAKUBWA WA HUDUMA YA AIRTEL MONEY

 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (kushoto) akiongea wakati  wa uzinduzi wa ushirikiano wa kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Makao makuu ya Airtel Morocco Jijini Dar es Salaam. pichani kulia ni mkuu wa kitengo cha IT Bank of Afrika bwn. Willington Munyanga , akifatiwa na  Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee  na anayefatia ni Meneja Airtel Money John Ndunguru.
 Meneja Airtel Money John Ndunguru na Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee  kwa pamoja wakikabidhiana mikataba mara baada ya makubaliano ya ushirikiano  wa Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika Makao makuu ya Airtel Morocco Jijini Dar es Salaam. wakishuhudia Katikati ni Mmoja ya wakala mkubwa wa Airtel money kutoka kampuni ya Connexions bwn Shyamkumar Balakrishnan (katika) na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
Meneja Airtel Money John Ndunguru na Mkuu wa huduma za kibenki Mwanahiba Mzee wakipitia mkataba mara baada ya makubaliano ya ushirikiano  wa Airtel na Bank of Afrika katika kutoa huduma ya Airtel money kupitia matawi ya bank hiyo yote yaliyopo Tanzania.
Reviewed by crispaseve on 09:14 Rating: 5

No comments

Post AD