LIGI KUU YA VODACOM SASA KATIKA SIMU YA MKONONI
Dar es Salaam 25, Oktoba 2012….. Mdhamini
Mkuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania, imewekeza katika kuwawezesha mashabiki wa soka kupata
taarifa na matukio ya mechi zote za ligi hiyo kupitia njia ya simu za
kiganjani na intanet.
Kupitia
mifumo mbalimbali ya kiteknolojia wateja wa Vodacom wataweza kupata
matokeo ya mechi mbalimbali kupitia simu zao za kiganjani ukiwa na
ujumbe mfupi wa maneno na mitandao ya kijamii.
Akizungumzia
hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema,
Mtandao wa Vodacom una miundombinu ya kutosha na unaongoza katika
masuala ya teknolojia. Hivyo itatumika katika kuwawezesha mashabiki wa
soka walioko ndani na nje ya nchi kujua matukio mbalimbali ya ligi kuu
ya Vodacom.
“Licha
ya ligi yetu kuonekana katika kituo cha Televisheni cha Super Sport.
Tumejipanga sasa kuhakikisha inakuwa katika mitandao mbalimbali muda
wote kwa kila mchezo na kila tukio katika soka, Mashabiki watapata
taarifa za ligi popote watakapokuwa,” alisema Meza na Kuongeza kuwa,
“Kupitia intanet matukio haya yatapatikana kupitia Facebook na Twitter
na mitandao mingine ya kijamii.”
“Ili kupata matokeo na taarifa mbalimbali kupitia njia ya simu mteja wa Vodacom atatakiwa kupiga *149*01# kisha atachagua VODACOM FLAVA na akisha kujiunga na huduma hiyo itakayo muwezesha kupata taarifa na matokeo ya mechi mbalimbali”
Aliongeza
kuwa, “ Kwa wateja wanaotumia facebook na twitter kwao ni rahisi zaidi
kwani huduma hizo zinatolewa bure na Vodacom, hivyo mashabiki wa soka
watatembelea Ukurasa wetu wa facebook na Twitter na kupata taarifa
mbalimbali kuhusu ligi na wengine kujishindia zawadi kwa kujibu maswali
mbalimbali zikiwemo tiketi za mechi za ligi,”
Aidha
Mkurugenzi huyo alitoa Pongezi kwa Vyombo vya habari kwa kazi kubwa
inayofanya katika kuwahabarisha watanzania kuhusu michezo mbalimbali
hususani ligi kuu ya Vodacom kupitia Televisheni, Radio, Magazeti na
Mitandao ya kijamii.
“Vyombo
vya habari ni wadau wakubwa na wanafanya kazi nzuri sana katika kutoa
taarifa hizi wanastahili pongezi, nasi tunaangalia namna ya kuwaunga
mkono kwa namna moja ama nyingine katika jitihada za kukuza soka la
Tanzania na tunaamini tutafika mbali.”
Mkurugenzi
huyo alihitimisha kwa kutoa pongezi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki
katika ligi kwa kusema kuwa zimeonesha hamasa kubwa na kubainisha kuwa
ni ishara ya ukuaji wa soka katika soka la Tanzania ambalo ndio lengo
kuu la Vodacom.
“Ligi
sasa imekuwa na msisimko kila timu inajitahidi kushinda kila mech,hadi
sasa timu zote zimeonesha kiwango kikubwa na soka la kuvutia tunatarajia
maendeleo haya yataleta tija hata kwa timu yetu ya Taifa kufanya
vizuri. Vipaji vingi vinaonekana na ajira kwa vijana imeongezeka kupitia
michezo,” alihitimisha Meza.
Kampuni
ya Vodacom katika kuongeza msisimko kwa mashabiki wa ligi imetoa ofa
mbalimbali msimu huu kwa kuwawezesha wateja wake kupata SMS 50, Muda wa
maongezi wa dakika 30 na MB 50 kwa shilingi 400 Ili kuwasiliana na ndugu
jamaa na marafiki. Pamoja na mambo mengine kampuni hiyo inaangalia
namna ya kutoa adha ya ukataji tiketi kwa wateja wake kutumia huduma ya M
- pesa kununua tiketi za mechi mbalimbali.
Kuhusu Vodacom Tanzania:
Kampuni
ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na
jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom
Foundation. Vodacom Foundation ina nguzo kuu tatu: Afya, Elimu na
Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo imechangia zaidi ya miradi 120
ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za
kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni
pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award
ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone .
Vodacom
Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania
inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Vodacom Tanzania ni
kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia
ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited
inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35 zilizobaki
zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa miaka mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.
Mwisho…….//////////
Reviewed by crispaseve
on
09:38
Rating:
Post a Comment