ABBEL DHAIRA: Ngongoti aliyetua Simba kumsaidia kazi Juma Kaseja
Abbel Dhaira |
Na Doris
Maliyaga, Muscat
SIMBA
imemnasa kipa imara tegemeo wa Taifa la Uganda, Abel Dhaira kwa ajili ya msimu
ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano mingine.
Ujio wa kipa
huyo katika kikosi cha Simba kutaleta uhai mpya kwenye eneo hilo kutokana na
uwezo wake katika kulinda lango.
Dhaira
atakuwa kipa mrefu zaidi kwenye Ligi Kuu Bara kwani kwani ana urefu wa zaidi ya
futi 6.5.
Mbali na
urefu alionao, amejengeka vizuri kimazoezi na ana umbo linalomfanya atishe awapo
langoni.
Kwa mdau wa
soka wa Tanzania, utamkumbuka Dhaira katika mashindano ya Kombe la Chalenji
2011.
Dhaira ndiye
alikidakia kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' katika mashindano
hayo na wao wakachukua ubingwa katika ardhi yao.
Uhodari wake
wa kupangua michomo ya penalti ndiyo iliwapa ubingwa huo katika mchezo wa
fainali walipocheza na Rwanda jijini Dar es Salaam. Uganda ilishinda kwa mikwaju
ya penalti 3-2 ambayo Dhaira aliiokoa baada ya matokeo ya awali kuwa sare ya
mabao 2-2.
Hakung'ara
katika mashindano ya Chalenji mwaka 2012 kutokana na kuwa majeruhi. Dhaira
alipata majeruhi katika mechi ya kwanza hatua ya makundi dhidi ya Ethiopia.
Aliumia
jicho la kushoto dakika ya 73 ya mchezo huo na kumfanya akose michuano hiyo
ambayo Uganda ilitetea taji lake.
Wakati wa
michuano hiyo ya Chalenji, Simba ilipata mwanya na kuzungumza naye akatua
klabuni kwao kwa ajili kuisaidia klabu hiyo katika Ligi Kuu na mashindano
mengine kama Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akiwa
kikosini hapo, Dhaira atasaidiana na makipa wengine, Juma Kaseja, Wilbert Mweta
na Wazir Hamad.
Kumbuka
Kaseja ndio amekuwa nguzo ya Simba tangu mwaka 2003 ingawa alihama msimu wa
2008/09 na kujiunga na Yanga.
Kaseja, hata
hivyo, alirejea Simba msimu uliofuata na ndio kinara wa timu hiyo hadi sasa.
Ujio wa
Dhaira ni changamoto kubwa kwa Kaseja, ambaye hajapata ushindani mkubwa wa namba
tangu ameanza kuchezea timu hiyo.
Dhiara
ambaye ana miaka 26 sasa, udogo wa umri alionao na kiwango chake wanaweza
kunufaika kwa namna nyingi katika udakaji wake.
Mara baada
ya kufika Tanzania kujiunga na kikosi chake, Mwanaspoti ilifanya mahojiano naye
kwa kina naye alieleza sababu ya kutua Tanzania.
Sababu ya
kutua Simba
"Simba ni
klabu kubwa lakini pia maslahi, tumekubaliana ndiyo maana nimekuja hapa na
naahidi kuitumikia kwa moyo mmoja kuona inafanya vizuri katika michuano
mbalimbali itakayoshiriki,"anasema Dhaira.
Utendaji
wake Simba
"Mungu ni
kila kitu. Nimekuja kucheza Simba nikiwa na matumaini ya kufanya vizuri na
naamini kila kitu kitakwenda sawa.
"Najiamini
na nimejipanga vizuri kuona naifanyia Simba kazi nzuri kwa sababu kufanya kwangu
vizuri ni kawaida.
"Nimekuwa
bora katika ligi ngumu ya Iceland nikiwa na IBV msimu uliopita kwa hiyo sioni
kama kutakuwa na cha ajabu kitakachonifanya nishindwe kufanya kazi
hapa,"anaeleza Dhaira huku akijiamini.
Kuhusu
ushindani wa namba: "Ushindani upo kila mahali na hakuna chenye kushindikana
mbele ya Mungu, hayo ni mambo ya kawaida kabisa kwa mchezaji.
"Sina
wasiwasi na jambo lolote ninachofanya ni kutimiza majukumu ya kazi yangu
iliyonileta,"anasisitiza Dhaira.
Hata hivyo,
Dhaira anasisitiza jambo moja juu ya mashabiki wa kikosi hicho kwa kusema:
"Nitafanya vizuri lakini mashabiki wa soka wa Simba na wengine wote, wanipe muda
katika kipindi hiki kama wiki mbili ili niwe vizuri.
"Unajua
nimekuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu kutokana na tatizo la jicho (anaonyesha)
nikawa nafanya mazoezi lakini si ya nguvu si unajua kuumwa tena.
"Kwa sasa
kwa sababu nimepona, nataka kufanya ya nguvu zaidi ili niwe vizuri na kufanya
kazi yangu kwa malengo.
"Mashabiki
wasiwe na wasiwasi na mimi kikubwa nahitaji ushirikiano wao wa hali na mali ili
mambo yaende vizuri."
Historia
Dhaira
amecheza soka katika mataifa mbalimbali kama Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo na Iceland kabla ya kujiunga na Simba msimu huu.
Akiwa na
Uganda ambako ndiko kwao, aliichezea Express 2006-2008 ambapo klabu hiyo
ilichukua ubingwa wa Uganda maarufu kama Uganda Cup mara mbili mfululizo.
Baada ya
hapo alihamia URA ambako pia walichukua ubingwa wa Ligi Kuu Uganda maarufu kama
Uganda Premier League msimu wa 2009 na msimu huo ndiyo akatimkia Congo kuichezea
klabu ya AS Vita.
Akiwa na AS
Vita walishiriki Kombe la Shirikisho hata hivyo walitolewa hatua ya awali na
2011 aliachana na Ligi Kuu Congo na akajiunga na IBV ya Iceland ambako alikuwa
akicheza na kiungo, Tonny Mawejje ambaye pia ni raia wa Uganda lakini mwenzake
ametolewa kwa mkopo kwenda Golden Arrows ya Afrika Kusini.
Mwaka 2013
amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya Ligi kuu Bara na
michuano mingine inayowakabili.
WASIFU
WAKE:
JINA: Abbel
Dhaira
KUZALIWA:
Septemba 9, 1987
ALIPOZALIWA:
Jinja, Uganda
NAFASI: Kipa
KLABU
ALIZOCHEZEA:
Mwaka
Klabu
2006-2008: Express (Uganda)
2008-2010: URA (Uganda)
2010-2011:
AS Vita (DRC)
2011-2012: IBV (Iceland)
Kuanzia
2013: Simba SC
(Tangu mwaka
2009, ameidakia Uganda mechi 21)
MAKALA HII IMETOKA GAZETI LA MWANASPOTI LEO
MAKALA HII IMETOKA GAZETI LA MWANASPOTI LEO
Reviewed by crispaseve
on
09:34
Rating:
Post a Comment