WAENDESHA BODABODA WASAJILIWA KWA MFUMO MAALUMU
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Alternative
Communication Bw. Emmanuel John katika picha ya pamoja na baadhi ya waendesha
bodaboda mara baada ya kusajiliwa na kukabidhiwa jezi jana kwenye ukumbu wa
Princess Sinza Mapambano, Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Vodacom Stratton Mchau akizungumza na waendesha
bodaboda ktk hafla hiyo.
Waendesha boda boda wa Kanda ya Temeke wakiwa katika mkutano
mkutano wa pande nne, ambao ni uongozi wa Alternative Communication, Jeshi la
Polisi, Vodacom na Bodaboda wenyewe.
Baadhi ya waendesha bodaboda waliokwisha jisajili katika
mradi huo wakiwa kazini kuliendeleza libeneke huku wakiwa na uhakika wa bima
pale inapotokea ajali.
ZOEZI la kuwatambua waendesha bodaboda na kuwasajili katika
mfumo maalumu wa kumbukumbu (database) liliendelea tena mwishoni mwa wiki
iliyopita ambapo safari hii waendesha bodaboda katika kanda ya Kijitonyama
wamesajili na kupewa mafunzo muhimu katika maeneo ya usalama barabarani,
ujasiriamali na bima.
Kufanyika kwa zoezi hilo hapo jana ni mwendelezo wa mchakato
unaofanywa na kampuni ya mawasiliano, masoko na matangazo ya Alternative
Communication ya jijini Dar es Salaam, ikishirikiana na jeshi la polisi, lengo
likiwa kuwasaidia waendesha bodaboda na abiria wanaotumia usafiri huo
kutambulika kwa urahisi inapotokea wamehusika katika matukio ya kihalifu.
Hatua hiyo ina kuja kufuatia madai kuwa baadhi yawaendesha
bodaboda wasio kuwa waaminifu hujihusisha katika matukio ya kihalifu au
kutumiwa na wahalifu kuvunja Amani na kupotea bila ya kutambulika.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Emmanuel John
Rutagonya, amesema jijini Dar es Salaam kwamba tayari kampuni hiyo imekwisha wasajili
bodaboda 3,000 katika mfumo huo. Ameongeza kwamba wale waliosajiliwa pia
watapata faida ya kupewa huduma ya bima ya afya, mafunzo ya usalama barabarani
na Ujasiriamali.
Mwenyekiti huyo mtendaji alisema wale wanaosajili wa katika
mfumo huo wanapewa koti (Reflectors) zilizo na namba ya usajili kifuani na
nyuma ya koti. Namba hiyo ni utambulisho kamili wa mwendesha pikipiki, pia
kwenye kofia zao (helmet) itabandikwa namba ya simu ya Kiongozi wa Chama cha
Waendesha Bodaboda husika.
“Mtu yoyote akiipiga namba ya chama cha waendesha bodaboda
na akataja namba ya usajili wa dereva wa bodaboda, mfumo utamtambua dereva huyo
mara moja.”Alisema.
Kwa upande wake Meneja Mauzo Kanda ya Kawe wa Kampuni ya
Simu ya Vodacom, ambao ni wadhamini wa mradi huu, Stratton Mchau, alisema
Vodacom imeridhishwa sana na mradi huu, na kwamba mbali na mambo mengine ya
kiudhamini, Vodacom pia itawateua baadhi ya madereva wa bodaboda kuwa mabalozi
wa bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kubwa ya simu nchini.
Waendesha boda boda wa Kanda ya Temeke wakiwa katika mkutano
mkutano wa pande nne, ambao ni uongozi wa Alternative Communication, Jeshi la
Polisi, Vodacom na Bodaboda wenyewe.
WAENDESHA BODABODA WASAJILIWA KWA MFUMO MAALUMU
Reviewed by crispaseve
on
09:17
Rating:
Post a Comment