FILAMU YA AISHA YAZINDULIWA KWA KISHINDO WILAYANI PANGANI
Filamu
iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe
31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la
UZIKWASA.
Aisha
ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia
aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa
kike. Filamu hizi ni ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika
kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama
'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.
Kabla
ya filamu ya Aisha iliyozinduliwa kwa kishindo hivi karibuni, shirika
la UZIKWASA tayari limeshatengeneza filamu nyenigne mbili ambazo ni
FIMBO YA BABA na CHUKUA PIPI, wengi wa waigizaji waliomo ni wasanii wa
vijijini.
Pia
filamu hizi zinatokana na maisha halisi na utafiti wa kina katika
jamii. Kwa nji hii UZIKWASA inahakikisha filamu zake zinaeleweka na
zinafanya kazi kama kioo wka jamii. Lengo ni tuone, tuguswe na hatimaye
tuchukue hatua ili kuleta mabadiliko.
Filamu
ya AISHA inamhusu mwanamke anayeishi mjini na kuamua kurudi kijijini
kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. Wakati anajikumbusha maisha yake
ya zamani, na kukutana na familia yake pamoja na marafiki, kunatokea
mkasa wenye athari kubwa katika maisha yake. Watu wangefumbia macho
mkasa huo, lakini Aisha anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki
yake.
Filamu
hii inahusu unyanyaa, aibu na wahanga kulaumiwa, na namna gani inazuia
wanawake na wasichana kusema wazi. Pia inahusu baadhi ya mamlaka na
viongozi kusita kufatilia ukiukaji wa haki za binadamu. AISHA imeongozwa
na mtaalamu maarufu Chande Omar, imetayarishwa kwa ushirikiano na
Kijiweni Production, imefadhiliwa na A. Schindler na Swiss Development
Cooperation (SDC) na kusimamiwa na shirika la UZIKWASA. Filamu ya aisha
ni kwa heshima ya wanawake wote waliopitia mikasa ya namna hii.
FILAMU YA AISHA YAZINDULIWA KWA KISHINDO WILAYANI PANGANI
Reviewed by crispaseve
on
09:15
Rating:
Post a Comment