EGETE UTURUKI HADI SAUZI, YANGA 3, LEOPARDS 2
Mshambuliaji
wa klabu ya Yanga, Jerryson Tegete amedhihirisha 'kuzaliwa' upya katika ufundi
wa kupachika mabao baada ya kuingoza vyema timu yake katika ushindi wa mabao 3-2
dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
Tegete
ambaye alionekana 'kupotea' katika upachikaji wa mabao, alianza kufunga katika
dakika ya 26 kwa njia ya penati ambayo ilitokana na wachezaji wawili wa Black
Leopards kumwangusha Haruna Niyonzima na baadaye, kufunga bao la tatu kwa mkwaju
wa mbali katika dakika ya 72 ya mchezo.
Wakiwa
Uturuki, Tegete aling'ara vilivyo katika ufungaji na kuwa mchezaji pekee
aliyerejea nchini akiwa na mabao mawili. Hali hiyo imemfanya mchezaji huyo kuwa
na ushindani mkali na washambuliaji wenzake wawili, Hamis Kiiza na Didier
Kavumbagu ambao wapo katika chati ya juu ya ufungaji katika ligi kuu ya Tanzania
Bara.
Tegete
alisema kuwa siri kubwa ya kurejea katika kiwango chake ni kufanya mazoezi ya
ziada na kujituma zaidi katika uwanja na hasa kutokana na mafunzo mazuri ya
kocha wake, Ernest Brandts. "Najifua zaidi katika mazoezi ya timu yangu na
sababu kubwa ni kutaka kurejesha namba katika timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa
Stars.
Didier
Kavumbagu (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Black Leopards, wakati wa Mchezo
huo, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Wachezaji
wa Yanga, wakishangilia bao lililofungwa na Jerry Tegete
Reviewed by crispaseve
on
09:36
Rating:
Post a Comment