Tanzania ya pongezwa kwa kutatua migogoro Afrika
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.
Anne Makinda akiwasili leo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na
kupokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Hemed Mgaza
(katikati) Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge na Makanu Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulizi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (Mb).
Kulia ni Mhe. Sadifa Juma Khamis, (Mb).Mhe. Spika ameongoza ujumbe wa
Wabunge watano kudhuria Mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Jukwaa la
Kibunge lanchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa PF
–ICGLR (Forum of Parliaments of International Conference on Great Lakes
Region – FP/ICGLR) mjini Kinshasa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.
Spika Makinda na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende (kulia) wakiingia kwanye mkutano huo.
Picha ya pamoja ya maspika, Sekretarieti pamoja washirika wa maendeleo wa FP-ICGLR. Picha na Prosper Minja-Bunge
Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Kimataifa ya nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu (FP-ICGLR) limeitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa juhudi inazozifanya kuleta amani barani Afrika.
Pongeli
hizi zimetolewa leo na jumla ya nchi wa kumi na mbili zinazounda Jukwaa
hilo kwenye mkutano wa tatu unaoendelea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC) zimewataja Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete pamoa na watanzania kama wapenda amani barania Afrika.
Hii
ni kutokana na viongozi hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya
DRC/Rwanda na kundi la M23, migogoro ya Afrika ya Kati, mgogoro wa
Sudani na Sudani Kusini, mgogoro wa Kenya baada ya uchaguzi mkuu na
mingine mingi. Pamoja na Tanzania, Afrika Kusini nay imepongezwa.
Bunge
la Tanzania limewkilishwa na Spika wa Bunge ambaye ameongoza ujumbe wa
wabunge watano ambao ni Mhe. Mussa Azzan Zunge, Mhe. Pauline Gekul, na
Mhe Sadifa Juma. Wengine ni Mhe. Mohamed Mbarouk na Mhe. Prudenciana
Kikwembe.
Reviewed by crispaseve
on
10:27
Rating:
Post a Comment