BABY MADAHA AMCHANA LIVE DIAMOND PLATNUMZ.
Baby Joseph Madaha maarufu kwa jina la (Baby Madaha) amesema
kwamba msanii mwenzake wa muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la
Diamond Platinumz si msanii bali ni mfanyabiashara.
Madaha amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kwamwe huwezi
kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa
na kazi kulingana na kipaji chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki
bali ni msanii ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
Baby madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli
za muziki amesema kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa
msanii wa matukio huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana
wenye majina makubwa hususn wasanii.
Akizungumza na kandili yetu katika mahojiano maalum leo baby
Madaha alisema kwamba, “Binafsi niliposikia kwamba Diamond anaumiza
kichwa kunasa penzi la msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la
(Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa sababu nilitambua kwamba soko lake
la muziki limeanza kushuka hivyo lazima atafute eneo lingine la
kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee kuwika”.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na
kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake
kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza
kuporomoka”alifafanua Baby Madaha.
BABY MADAHA AMCHANA LIVE DIAMOND PLATNUMZ.
Reviewed by crispaseve
on
22:20
Rating:
Post a Comment