Header AD

KANYE WEST AIBWAGA NIKE NA KUSAINI MKATABA NA KAMPUNI YA ADIDAS

Confirmed Kanye West Signs to adidas
Hatimaye mwanamuziki Kanye West ameamua kutema dili na kampuni ya Nike aliyokuwa ameingia nayo mkataba hapo awali iliyokuwa kimtengenezea rapa za Nike Air Yeezy Era, Rapa huyo ambaye kwa sasa amesaini dili nono na kampuni ya ADIDAS aliweza kufunguka mengi kupitia mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha radio cha Hot 97 pamoja na BBC.
Katika mahojiano hayo Kanye west alinukuliwa akisema kwamba mkurugenzi mkuu wa NIKE Mark Parker alimuhaidi kumtengenezea matoleo mawili kila mwaka sambamba na nguo ambazo angekuwa akizibuni yeye mwenyewe lakini akasema anachoangalia ni maslahi na sio hivyo vitu huku akitoa mfano wa mcheza kikapu kama Michael Jordan kulipwa Dola Milioni 100 kila mwaka ikiwa ni takribani 5% ya shea yake na NIKE, taarifa zinasema kwamba kulingana na maslahi anayohitaji Kanye kutoka Nike isingeweza kumtimizia kutokana yeye sio mwanamichezo professional ndipo Rapa huyo akaamua kumwaga wino wake na kampuni ya ADIDAS huku chanzo kikubwa kikiwa ni suala zima la maslahi, Kampuni hizi mbili ya Nike pamoja na Adidas ni kampuni zilizopo katika ushindani mkubwa huku zikitengeza bidhaa mbalimbali kama viatu, soksi, tshirt, vest, mipira na vifaa mbalimbali vya michezo.
Reviewed by crispaseve on 13:07 Rating: 5

No comments

Post AD