MHE. UMMY MWALIMU AFUNGUA KIKAO KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA DEMOKRASIA KATIKA NGAZI ZA CHINI KWA MTIZAMO WA KIJINSIA
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akifungua kikao cha majadiliano ya taarifa juu ya Utafiti Kuhusu Hali ya
Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa kijinsia.
Naibu
Waziri wa Maendeleo Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefungua
kikao cha Kujadili Matokeo ya Utafiti wa Hali ya Demokrasia katika ngazi
za chini kwa mtizamo wa Kijinsia.
Kikao hicho kimeandaliwa
na Kituo cha Demokrasia nchini kwa ushirikiano wa Shirika la Kimataifa
la IDEA, na kuvishirikisha Vyama vya siasa, Wizara, Halmashauri na
Baadhi ya Taasisi Zisizo za Kiserikali.Kuijadili taarifa hiyo.
Wakati
akifungua kikao Mhe.Ummy amesisisitiza kuwa, Demokrasia kamili haiwezi
kupatikana bila ushiriki sawa wa wanaume na wanawake na kuongeza kuwa,
Serikali za mitaa ni wadau wakubwa wa kuleta usawa wa demokrasia.
Mwenyekiti
wa kikao hicho Mhe. Ibrahimu Lipumba akitoa taarifa za Awali za Matokeo
ya Utafiti huo. Mhe.Lipumba amesema Utafiti huo ulihusisha madodoso mia
sita(600) kutoka katika Mikoa minane nchini.
Mwakilishi
kutoka Shirika la Kimataifa la IDEA ndugu Rumbidzai Kandawasvika Nhundu
akielezea matokeo ya Utafiti uliofanywa kwa ushirikiano wa Kituo cha
Demokrasia na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa kikao wakati wa majadiliano.
Baadhi ya Washiriki wa kikao wakati wa majadiliano.
Washiriki
wa kikao cha kujadili Matokeo ya Taarifa ya Utafiti wa Hali ya
Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa Kijinsia katika picha ya
pamoja.
MHE. UMMY MWALIMU AFUNGUA KIKAO KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA DEMOKRASIA KATIKA NGAZI ZA CHINI KWA MTIZAMO WA KIJINSIA
Reviewed by crispaseve
on
00:03
Rating:
Post a Comment