Header AD

Miaka 10 ya onyesho la ‘Lady in red’ Februari 14, Wabunifu mbalimbali kupamba



Na Mwandishi Wetu

WABUNIFU mbali mbali kupamba  miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in Red Super  brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika Februari  14,  ambapo pia litatumbuizwa na burudani kutoka kwa  Babloom Trio bendi na Wanne Star, kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo, Asia Idarous Khamsin, alisema tayari maandalizi ya onyesho hilo yameshakamilika na tayari wabunifu mbalimbali wameanza mchakato wa kuandaa  mavazi yao watakayoonyesha siku hiyo.

Asia Idarous alipongeza wadau mbali mbali  kwa kuliunga mkono onyesho hilo la ‘Lady in red’ hadi kufikisha miaka 10, tokea kuanzishwa kwake, na kutamba kuwa la kipekee kwa mwaka huu. “Februari  14, mwaka huu ndiyo siku pekee kwa wadau wa mitindo na urembo ambapo watashuhudia wabunifu mbalimbali siku hiyo wakipamba jukwaa, wakiwemo wakongwe na wale wanaochipukia” alisema Asia Idarous.

Na kuongeza kuwa, kwa mwaka huu wametoa fursa kwa wabunifu wanaochipukia kuonyesha mitindo yao sambamba na wakongwe ili kuleta changamoto kwen ye tasnia hiyo ya ubunifu na mitindo hapa nchini.
Aidha, katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya Februari 14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s  Day’ , kiingilio kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum ikiwa sh 50,000, ambapo pia kutakuwa na burudani kutoka bendi ya Babloom Trio  na Mwanamuziki  mahiri wa nyimbo na ngoma za asili, Wanne Star.

 Asia Idarous aliyashukuru makampuni mbalimbali ambayo yamejitokeza kudhamini onyesho hilo wakiwemo kampuni ya nywele ya Darling-‘Quality hair additions’,  na  Zanzi ‘Cream liqueur’ ambao ni wadhamini wakuu mwaka huu. Wengine ni  CXC, Times fm, Clouds media, Vijimambo blog, michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution, Raysa Style,Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View Vayle Spring, Voice of American na mengine mengi.
Miaka 10 ya onyesho la ‘Lady in red’ Februari 14, Wabunifu mbalimbali kupamba Miaka 10 ya onyesho la ‘Lady in red’ Februari 14, Wabunifu mbalimbali kupamba Reviewed by crispaseve on 21:01 Rating: 5

No comments

Post AD