MOVIE REVIEW: BARKHAD ABDI, NYOTA ALIYEWEZA KUUVAA UHALISIA KATIKA FILAMU YA "CAPTAIN PHILIPS"
Barkhad Abdi ambaye ameigiza kama Abduwali Muse Kiongozi wa Kundi la Maharamia katika Filamu ya Captain Philips.Imeandikwa na Josephat Lukaza Kwa Msaada wa Mtandao.
Filamu
ijulikanayo kama Captain Philips ni Moja ya Filamu iliyotoka mnamo
tarehe 11 Ocktoba 2013, Filamu hii imeongozwa na muongozaji mahiri
kabisa kutoka Hollywood aitwaye Paul Greengrass. Pamoja na
Kuiongoza Vyema Filamu hiyo lakini filamu hiyo ni moja ya filamu
iliyotumia Kiasi cha Dola Za Kimarekani Milioni 55.
Filamu hii ya Captain Philips Imeandikwa kutoka kwenye kitabu Kijulikanacho kama "A Captain's Duty: Somali Pirates, Navy SEALs, and Dangerous Days at Sea" ambacho kimeandikwa na Richard Phillips pamoja na Stephan
Talty. Filamu hii imetengenezwa kutokana na Tukio halisi la kutekwa kwa
Meli ya MV Maersk Alabama Mnamo mwaka 2009 na kupelekea Nahodha wa Meli
hiyo iliyotekwa mnamo 2009 Captain Richard Philips kushikiliwa na
maharamia kwa kile kinachodaiwa Kuwa Wabadilishane ili kuweza kulipwa
Pesa za Kimarekani.
Ni Filamu iliyochezwa na Tom
Hanks kama ndie captain Philips huku akikinzana na Muigizaji mahiri
mwenye Asili ya Somalia Barkhad Abdi ambaye alitumia jina la Abduwali
Muse kama kiongozi wa Maharamia ambaye Mwishoni aliweza kushikiliwa na
Jeshi la Maji la Marekani baada ya kudanganywa kupanda kwenye meli ya
Kijeshi ya Marekani ijulikanayo kama USS Bainbridge kwaajili
ya kukubalia juu ya Kiasi cha Pesa walichokuwa wakikitaka kwaajili ya
kumuachilia Captain Philips ambaye walimshika Mateka. USS Bainbridge ni meli ya kijeshi ambayo
ilikuja kutoa msaada mara baada ya Captain Philips Kuomba Msaada katika
Kituo Cha Kijeshi cha Majini Kinachopamba na Maharamia kilichopo
Dubai.
Ni
moja ya Filamu ambayo kikukweli ukiitazama kwanza huwezi kuboreka, Pili
rangi iliyotumika katika Filamu hiyo Ni Nzuri sana , Huku sauti zikiwa
zinasikika vizuri kabisa.
Lugha zilitumiwa katika filamu hii ni Kiingereza na Kisomali.
Ufuatao ni Wasifu wa Muigiza Barkhad Abdi ambaye aliigiza kama Abduwali Muse kiongozi wa Maharamia walioteka Meli ya MV Maersk Alabama
Jina kamili: Barkhad Abdi
Amezaliwa: April 10, 1985
Makazi yake: Minneapolis, Minnesota
Uraia: Mmarekani Mwenye Asili ya Kisomali
Kazi yake: Muigizaji, Mtayarishaji na Muogozaji wa Filamu na Muziki
Tuzo alizowahi kuchukua ni Kama Capri
Breakout Actor Award, Indiana Film Critics Association Award for Best
Supporting Actor, Boston Society of Film Critics Award for Best
Supporting Actor (2nd place), Dallas-Fort Worth Film Critics Association Award for Best Supporting Actor (3rd place), National Society of Film Critics Award for Best Supporting Actor (3rd place) na nyingine Nyingi tu.
Kabla ya Kuingia kwenye Tasnia ya Filamu Barkhad Abdi alikuwa
ni Dereva na Mtunza store ambaye alijiajili mwenyewe katika Biashara ya
Mawasiliano ambapo ofisi zake zilikuwa katika Jengo la Marekani (Mall
of America) akiwa pamoja na kaka yake Guled Abdi.
MOVIE REVIEW: BARKHAD ABDI, NYOTA ALIYEWEZA KUUVAA UHALISIA KATIKA FILAMU YA "CAPTAIN PHILIPS"
Reviewed by crispaseve
on
23:25
Rating:
Reviewed by crispaseve
on
23:25
Rating:

Post a Comment