PICHA MAALU KUTOKA JESHI LA MAGEREZA:ALIYEKUA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI DKT. EMMANUEL NCHIMBI AKABIDHI OFISI RASMI KWA WAZIRI MPYA WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI MHE. MATHIAS CHIKAWE, LEO JIJINI DAR
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi
akitoa neno fupi wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano rasmi ya Ofisi kwa
Waziri Mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mhe. Mathias Chikawe(wa pili
kulia). Hafla hiyo imefanyika leo Januari 27, 2014 katika Ukumbi wa
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe
akitoa maelezo mafupi mbele ya Waandishi wa Habari kabla ya kumkaribisha
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi
katika hafla fupi ya Makabidhiano ya Ofisi leo Januari 27, 2014 Jijini
Dar es Salaam.

Baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Idara zilizo
chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza aliyekuwa Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi wakati wa hafla
ya Makabidhiano rasmi ya Ofisi leo Januari 27, 2014 Jijini Dar es
Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John
Casmir Minja.

Baadhi ya Watumishi Waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
wakimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt.
Emmanuel Nchimbi(hayupo pichani) katika hafla fupi ya Makabidhiano rasmi
ya Ofisi leo Januari 27, 2014 Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza
PICHA MAALU KUTOKA JESHI LA MAGEREZA:ALIYEKUA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI DKT. EMMANUEL NCHIMBI AKABIDHI OFISI RASMI KWA WAZIRI MPYA WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI MHE. MATHIAS CHIKAWE, LEO JIJINI DAR
Reviewed by crispaseve
on
23:20
Rating:

Post a Comment