Header AD

Waziri Muhongo apata ugeni kutoka nchini Ufaransa


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri) pamoja na Waziri Mstaafu wa Viwanda na Nishati wa Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi), pamoja na watendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa na Wizara ya Nishati na Madini, wakati walipomtembelea wizarani ili kufahamu fursa za uwekezaji katika sekta hizo.
Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) , Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri), Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi), pamoja na mtendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini, wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyolenga katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini nchini.

Na Teresia Mhagama

Balozi wa Ufaransa nchini Bw. Marcel Escure akiongozana na  Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa,  Bw. Erick Besson wamemtembelea wizarani Waziri wa Nishati  na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ili kufahamu fursa za  uwekezaji katika sekta za Nishati na Madini. Waziri huyo mstaafu wa Ufaransa, Bw.Erick Besson alikuwa  akiiwakilisha kampuni ya GDF Suez ya Ufaransa. Katika suala la usimamizi wa bomba la gesi asilia, Profesa  Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la Maendeleo  ya Petroli (TPDC) litahitaji kupata uzoefu na pengine mbia  liyebobea katika usimamizi wa bomba hilo atakayeshirikiana na 

TPDC katika usimamizi wa bomba la gesi nchini. 
Kuhusu umeme, Waziri Muhongo alimweleza Waziri mstaafu  huyo wa Ufaransa kwamba serikali inajikita katika miradi ya  usambazaji umeme kwa utaratibu wa ubia au mikopo ya bei nafuu  na ina mpango wa kujenga njia ya umeme ya msongo wa 400kv  kuelekea ziwa Tanganyika hivyo aliikaribisha kampuni ya GDF  Suez kuwekeza katika miradi hiyo ya usambazaji umeme.Aidha Profesa Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la  Madini la Taifa (STAMICO) linatafuta mbia watakayeshirikiana  naye katika kuendesha mtambo wa kuzalisha umeme kwa  kutumia makaa ya mawe, Kiwira mkoani Mbeya hivyo kama wana  nia ya kuwekeza katika eneo hilo pia wanakaribishwa kuingia  katika ushindani wa kupata nafasi hiyo.

Naye Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa, Bw. Besson alimshukuru Profesa Muhongo kwa taarifa nzuri kuhusu fursa za uwekezaji nchini na ameahidi kupata taarifa zaidi za uwekezaji katika mashirika ya TPDC, STAMICO na  TANESCO ili kuona jinsi kampuni ya Suez itakavyoshirikiana na  mashirika hayo katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini.
Waziri Muhongo apata ugeni kutoka nchini Ufaransa Waziri Muhongo apata ugeni kutoka nchini Ufaransa Reviewed by crispaseve on 05:29 Rating: 5

No comments

Post AD