KAMPUNI YA ISSERE SPORTS YATOA JEZI KWA SHULE YA SEKONDARI YA KEREZANGE
Mchezaji
wa zamani wa Simba, Qureshy Ufunguo (Kushoto) akimkabidhi jezi namba 14
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kerezange, Kivule Ilala Dar es Salaam, Bi.
Kirundu Mgeni kwa niaba ya Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere
Sports, Abbas Isere kwa ajili ya timu ya soka shuleni hapo, Issere
Sports ilitoa jezi mipira miwili na soksi (Picha na Mpigapicha Wetu)
KAMPUNI
ya kuuza vifaa vya michezo, Issere Sports imetoa jezi mipira na soksi
kwa timu ya soka ya Shule ya Sekondari Kerezange, iliyoko Kivule Ilala,
Dar es Salaam.
Akikabidhi
jezi hizo mchezaji wa zamani wa Simba, Qureshy Ufunguo aliyemwakilisha
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Issere, Abbas Ally alisema michezio
inafanya wanafunzi kuondokana na maradhi.
Ufunguo
aliyekubali kufundisha timu ya soka ya shule katika mashindano ya shule
za Sekondari (UMISETA) alisema atatumia uwezo wake kuhakikisha timu
hiyo inafanya vizuri katika mashindano hayo.
Mkuu
wa Shule hiyo. Kirundu Mgeni alisema vifaa hivyo ni chachu ya wachezaji
wa shule yake kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya ndani na
nje ya wilaya yao ya Ilala.
Awali
Mwalimu wa michezo wa shule hiyo, Baraka Mololo alisema shule yake ina
wachezaji wengi wenye vipaji ambao wakiendelezwa wanaweza kuchezea timu
za Simba na Yanga na hata Taifa.
Alisema
hivi karibuni shule hiyo ilifanya vizuri katika mashindano ya kirafiki
na shule za jirani na kuibuka washindi hivyo ana matarajio makubwa ya
kutwaa ubingwa wa UMISETA mwaka huu.
KAMPUNI YA ISSERE SPORTS YATOA JEZI KWA SHULE YA SEKONDARI YA KEREZANGE
Reviewed by crispaseve
on
05:30
Rating:
Post a Comment