DARREN BENT AINYIMA USHINDI MAN UNITED DAKIKA YA MWISHO KABISA OLD TRAFFORD
BAO
la dakika ya mwisho la Darren Bent limeinyima ushindi Manchester United
baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani Uwanja wa Old Trafford na
Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Baada
ya Fulham kupata bao la kuongoza kupitia kwa Steve Sidwell dakika ya
19, United ilipata mabao mawili ya haraka haraka na kuongoza mchezo
kupitia kwa Robin van Persie dakika ya 79 na Michael Carrick 80.
Matokeo
haya yanaifanya United ya David Moyes ijiongezee pointi moja na
kufikisha 41 baada ya kucheza mechi 25, ikiendelea kubaki nafasi ya
saba.
Nafasi
ya mwisho: Manchester United ilikomolewa dakika ya mwisho kabisa kwa
bao Darren Bent na kulazimishwa sare ya 2-2 na Fulham
Mambo
magumu: David Moyes kichwa kinamuuma United pamoja na jitihada zote
ikiwemo kumsajili Juan Mata kutoka Chelsea, lakini mambo bado magumu
DARREN BENT AINYIMA USHINDI MAN UNITED DAKIKA YA MWISHO KABISA OLD TRAFFORD
Reviewed by crispaseve
on
00:15
Rating:
Post a Comment