MILEY CYRUS AUMIZA KINYWA CHAKE KWA TATTOO MPYA ALIYOCHORA KWENYE LIPSI.
Duh! Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi, Dunia inaelekea
mrama kutokana na vihoja vinavyoendelea kutokea kila kukicha hiyo
inakuja kufuatia Mwanamuziki wa kibao cha ‘Wrecking Ball’ mwendawazimu
‘Miley Cyrus’ kuja na kioja cha aina yake baada ya kuamua kuumiza lipsi
zake na kujichora tattoo ya rangi kwa kimombo ‘colorful tattoo’ na
kisha kutupia picha hiyo mtandaoni iliyoambatana na ujumbe uliosomeka
“#sadkitty #f–kyeahtulsa,” Cyrus, 21”..

Pichani ni Miley Cyrus akionyesha Tattoo yake mpya aliyoichora kwenye Lipsi zake iliyo na picha ya mtoto wa paka ‘Kitty’
Tangu kuanza kwa ziara yake ya muziki iliyopewa jina la
BANGERZ, , Miley amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wake hasa
kutokana na mfululizo wa vituko anavyokuwa akivifanya pindi anapokuwa
jukwaani, mojawapo ya tukio lililovuta vichwa vingi vya habari na
kuandikwa sana mitandaoni ni kitendo chake cha kukutanisha ndimi na
mwanamuziki ‘Katty Perry’ alipokuwa akiperform katika ukumbi wa Staples
Center Los Angels mwezi uliopita.
MILEY CYRUS AUMIZA KINYWA CHAKE KWA TATTOO MPYA ALIYOCHORA KWENYE LIPSI.
Reviewed by crispaseve
on
05:57
Rating:
Post a Comment